NASHUKURU FIESTA NA CLOUDS MEDIA KWA KUNICHAGUA KUWA MMOJA KATI YA WALE WENGINE WALIOCHAGULIWA PIA NA KUNIPA TUZO HII

Na nitake radhi kwakuwa sikuweza kuhudhuria, kutokana na kuwa nipo safarini
Ila nimeshukuru sana kwa kupewa heshma hii, na ninashukuru pia hata nisipokuwepo lakini wapo watu wa kunipokelea.

Iko katika mikono salama na nikirudi nitaibusu na kupiga nayo pichaNimshukuru MUNGU pia kwa kunipa Nuru inayosababisha wengine pia wananiona
Manake angeamua kunipa giza nisingeonekana
Nakuheshimu sana SIR GOD, nakurudishia sifa na utukufu pia.

Watu wangu eeh, birthday ya mwakani zawadi naomba iwe Kabati la trophies
Lile lililoko Home, limejaa!!!

Asante kwa Bi. Linah pia kwa kuniheshimu na kuniona kama mfano na kuimba wimbo wa MACHOZI.

Inaniogopesha sana wakati mwingine watu wengi wadogo kwangu wakiniona kama mfano nafikiria nikianguka sijui na wao nitakuwa nimewaangusha??
Mbarikiwa sana na tuzidi kuombeana kwa Mola
Kila lililoandikwa lazima litimie
Mpaji ni MUNGU na siku hazigandi.

Nawaombea pia mfike mbali zaidi ili mtusaidie pia tulioanza mahali tutakapokwamia

Shaa, Mwasiti, Kaysha, Linah na wengine wote wadogo ambao nimesahau kuwataja lakini mko moyoni mwangu. Nawaambia neno moja tu
HAKUNA KURUDI NYUMA!!! No matter what.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive