GARLIC POTATOES

Unaweza kula na beef, fish, chicken au hata VegiesJinsi ya kupika viazi hivi vya Garlic

Hatua ya 1. Andaa kila kitu kwanza kuliko kuanza kukimbia kimbia wakati wa kupika

Unakata kata mbwembwe za aina tofauti katika vipande vidogo vidogo sana

Karot, Hoho za rangi rangi, Vitunguu maji na Vitunguu Thaumu vya kuponda vya kutoshaHayo ndio mahitaji ya mwanzoHatua ya pili ni kuviosha viazi na kuvikata vipande vidogo vidogo kwa ukubwa wa kiazi kimoja kupita mdomoni kwa wakati mmojaWeka maji kiasi kidogo kama kikombe kimoja na nusu, weka chumvi kisha chemsha mpaka viive wasnani bila kumomonyoka na kuanza kutoa unga ungakisha vitoe jikoni umwage maji yoyote yaliobaki na kuviacha vikiwa vikavuHatua inayofuata ni kuweka Butter katika kikaango nakuikaanga kwa muda wa dakika mojaIkianza kuyeyusha unaweka viazi pamoja na mboga mboga zote zilizokatwa, hakikisha Garlic inajitokeza zaidi maana ndio yenye kuleta ladhaUnavikaanga kwa dakika 5 -7 mpaka vichanganyike vizuriKisha unaweka maziwa ya maji vijiko 5 unaacha kidogo yachemkie mpaka yakauke, hii ni kwa viazi 3 vikubwa ambavyo huwa ni portion ya mtu mmoja

Ukipakua inaonekana hivi, ukila sasa ndio usiseme

Wengine hukamulia na ndimu au Limao kwa juu, kutokana na upendeleo wa ladha ya mtu mdomoni kwakeVinapatikana pia Nyumbani LoungeNo comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive