Diet" DAY 7 "Siku Hii wanaopenda kula Watafurahi"Siku ya saba naiandika kwa Confidence kwakuwa haina milima wala mabonde emengi sana kama vipo ni vya kuvikabili.

Asubuhi usiache kufanya mazoezi hata iweje. Tembea dk,30 -45

Ukiwa na partner inaweza kuwa rahisi mkiwa mnasindikizana huku mnapiga story inasaidia kujisahau na kustukia muda umeisha.Kama huna hata peke yako haina tatizo, maadam umeamua.

Ukirudi fanya sit ups nyingi kwa kadri ya uwezo wakoKunywa maji ya moto/ vuguvugu Glass 4 kama kawaida

Kikombe kimoja cha Chai au kahawa,

Yai moja la kuchemsha na maziwa Glass mojaVipi! kuna unafuu kidogo au bado sana?

Kabla ya kula Lunch: Kunywa tena maji moto/vuguvugu glass 4

Halfu unywe Vegetable Noodle Soup pamoja na ndizi moja ya kuchemsha "Bukoba"

Sio zile ndizi za sukari.Baada ya hapo kula matunda mengi sana ya kutosha, hata ukila ndizi mbivu pia kwa leo ni sawa tu

Hii ishu hapo juu iache kwanza

Jua likizama tembea dk.30-45 ukirudi fanya sit-ups ingia bafuni kuogaUsiku ni wakati wa BBQ, wakati unangojea huku unazungumza unakunywa maji moto/vuguvugu glass 4.Kama utachoma BBQ nyumbani ni sawa, kama utaagiza kutoka nje pia ni sawa

Ila kwa muda ule wakati unasubiri mlo unweza kunywa hayo majiKwasababu kuchoma nyama sio kitu rahisi sana na sio kila mtu anajuaSiku ya 7 unatakiwa kula nusu kuku kwenye Dinner yako, ila sio lazima umalize

"Hiyo mishkaki haipo kwenye diet, usiihesabu"

Unatakiwa pia ule Salady ya aina yoyote ile kwa wingi wowote ule

Ususahau kuomba dua pia kabla hujalaLeo ni wali maharage, Nusu kuku au "Beef Sausage" na salady kwa DinnerUnaruhusiwa kunywa glass 2 za white wine baada au wakati unakula kama ni KUKU

Au glass 2 za redwine baada au wakati unakula kama ni Beef Sausage

Ila kama ni Kuku iwe Kuku

Kama ni Beef sausage iwe hiyo na sio vyote viwiliKwa hii siku ya 7Wine mwisho ni glass 2 tu

Manake ukifanya komeshea ukalewa kesho yake utashindwa kuamka asubuhi na hutaweza kuendelea na diet kwakuwa.Kwanza unaweza kuwa na hang over itakayokupelekea uanze kutafuta vyakula vingine tofauti na mtiririko wa hatua hii tunayopitia.

Pia ukichelewa kuamka hutoweza kufanya mazoezi na uta skip moja ya mlo wa sikuJiandae ya siku ya 8 ni ngumu zaidi, baada ya kuji spoil na week endNo comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive