MAPISHI MENGINEYO YA KUKU

Kuna mapishi mbali mbali ya kuku.
Na kila moja lina utamu na tofauti yake.
Hili ni langu jingine, ukilipenda fuatilia kanuni hizi ili litokee ipasavyo.

Unakata Kuku vipande vya wastani kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu
Unamuosha vizuri, unaacha akauke maji.
Unapaka chumvi na ndimu / Limao unanyunyizia na black pepper kwa mbali
Unamuacha kwa muda kama wa dakika 20 viunge viingie ndani ya Nyama

Vitu vinavyotakiwa kuwa vimeandaliwa kwaajili ya kuweka kwenye kuku ni
Hoho za rangi, kijani, njano na nyekundu
Karoti, Kitunguu maji, Tangawizi ilikatwa vipande bila kusagwa, na Vitunguu thaumu vilivyokatwa vipande bila kusagwa na nyanya moja

Si vibaya pia ukiwa unapika huku unakula muziki kupitia ka radio kadogo kwa pembeni

Hatua inayofuata ni kuweka mafuta kidogo sana ya alizeti kwenye kikaango
Yakipata moto wa kutosha unaweka kuku unaacha mpaka wapate rangi ya brown ukiwa unawageuza geuza. Ila hakikisha mafuta si mengi " Hii sio deep fry"

Kuku wakisha kuwa brown unaweka viungo vyako vyote kasoro nyanya
Unaacha vichemkie kwa dakika 5 -7 kisha unaweka nyanya unafunikia tena kwa dakika 5-7

Halafu unaweka soya sauce na pilipili kama unapenda
Kama hupendi hivyo vitu vya mwisho si lazima kuweka
Unaweza kuongezea flavor nyingine yoyote ile unayoipenda kwa finishing
Baada ya hapo kuku anaonekana hivi na anakuwa tayari kuliwa
Sio kila siku tu ma michuzi michuuuuuuuuuuuzi
Mi sipendi michuzi

Kuku kama huyo unaweza kumla na wali, ukasindikizia na mboga nyingine kama maharage au kabichi au kingine chochote, Spinach, Mchicha, Bamia n.k

Alieomba recipe ya biriani kuna mahala nimegelezea nita paste na kutoa credit kwa alienitumia kuanzia jumatatu. Weka macho wazi

Kwa sasa hilo jiko ndilo ninalotumia kwa kupikia chakula
Sio jiko langu, ila hapo ndipo ninapoishi kwa sasa


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive