NAUNGANA NA WATANZANIA WENZANGU KUTOA POLE KWA WENZETU WALIOFIKWA NA MAAFA NA WALIOONDOKEWA.....MUNGU azilaze roho za marehemu pema peponi, Amen

Mbali na mimi kuna watanzania wengine pia wametoa salaam za pole

TMTV a.k.a TANZANIA MUSIC TELEVISION
TUNATOA SALAMU ZETU ZA POLE KWA WATANZANIA WOTE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA KUFIKWA NA MSIBA MKUBWA HUU WA KUZAMA KWA MELI YA MV.SPICE ISLANDER AMBAO UMEPOTEZA MAISHA YA MAMIA YA WATU NA KUWAACHA WENGINE MAJERUHI.

TUNAWAOMBEA MAJERUHI WOTE KWA ALLAH WAPONE KWA HARAKA,

PIA MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI WALE WOTE WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO.
AMIIN.
TMTV a.k.a TANZANIA MUSIC TELEVISION
UTAWALA

Kwa niaba ya jumuiya ya watanzania waliopo nchini uingereza chini ya Mwenyekiti wa TANZ- UK taifa imesikitika sana na kuwapa pole watanzania wenzetu wa zanzibar kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa. Watanzania wote tulio hapa tunaungana nanyi kwa pamoja katika wakati huu mgumu na pia tuko tayari kushirikiana kwa hali na mali kuwafariji ndugu na jamaa kwenye msiba huu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

Mwenyekiti TANZ- UK.
Dr John Lusingu

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive