KUMBUKUMBU YA 4 YA MZEE SHAURI TIMOTH NATHAN NA PIA NI SIKU YA KUZALIWA MWANAE "Mroki Mroki"

Huyu ni mwana, Mroki T Mroki, almaarufu kama Father Kidevu.
Alizaliwa Tar 18 Septembre

Na huyu ni baba , Mzee Nathan alifariki tar 18 Septembre miaka 4 iliopita. RIP

Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika minne sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 - 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/09/2007 saa kumi na mbili jioni.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.

Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Timothy Kille, Maria Thomas Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan Dossa, Dinner Onesmo, Debora Daniel na Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani na Shauri.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana.

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive