NIMEPATA DIET NYINGINE RAHISI YA KUPUNGUZA MWILI NA TUMBO LA CHINI KWA WANAWAKE....Inaenda kwa mwezi mmoja" Ukipenda kufuatilia tuanze wote leo"

Kuna njia nyingi sana ambazo watu huwa wanajaribu ili kupunguza mwili na tumbo lakini either zinakuwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanamoishi hivyo kupelekea kushindwa njiani.



Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu.

Kwakuwa kahawa huwezi kutumia zaidi ya round 3 kwa maana hiyo ukinenepa tena inabidi utafute njia nyingine.



Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka mwili.

Mara nyingi vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa ndio vinatuponza



Sasa, je! Unaweza kujaribu kuishi hivi bila ku cheat hii process???





Siku ya kwanza, ukiamka tu kitandani ukapata nguvu kabla ya kufanya chochote jivalie raba zako na nguo za mazoezi. Jaribu kutembea dakika 15 toka nyumba unayoishi na dakika 15 kurudi nyumba unayoishi hapo jumla utakuwa umetembea kwa miguu kwa dakika 30.





Na kama mkakati wako ni kupunguza Tumbo pia, Ukirudi fanya sit-ups 15 -20 kwa siku ya kwanza. Ukiona ni ngumu unaweza kujaribu kuanza hata na 10. Utaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utakavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu.



Unaweza kutumia Bench au unaweza kulala sakafuni

Kwa wanaoishi Dar es Salaama ma bench ya Sit ups yanapatikana Shopperz Plaza kwenye duka la vifaa vya michezo



Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4

Sio lazima uyanywe yote kwa wakati mmoja

Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glass 4 ziishe

Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu



Limao na ndimu sio tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini



Baada ya hapo unaruhusiwa kwenda kuoga, na kujiweka sawa ila usipige mswaki

Nitakwambia kwa nini!!


Kunywa breakfast yako:

Unaruhusiwa kunywa kikombe 1 cha kahawa au Chai lakini usiweke zaidi ya kijiko 1 cha sukari

Unaruhusiwa kula yai 1 tu la kuchemsha



Mikate hii ya brown mimi siipendi na wala haina ladha nzuri lakini utafanyaje maadam unataka lako la kuepuka unene yabidi ule tu.



Slice 1 tu ya brown bread tena iwe toasted, usithubutu kuweka Siagi wala vinavyofanana na hivyo

Matunda jimiminie kadri uwezavyo, epukana na ndizi tamu

Baada ya hapo unaweza kupiga mswaki sasa na kuendelea na shughuli zako

Ila kabla ya kuendelea na shughuli zako ni lazima utaenda haja kubwa

Ndio lengo hasa la kutopiga mswaki kabla ya breakfast



Lunch:

Kula upande wa kuku Robo, 1/4 my friend kama ni upande wa paja ndio uliochagua

Kuku unaetakiwa kula ni lazima awe wa kuchoma au kuchemsha na si vinginevyo



Ukitaka upande wa kipapatio ndio utakao kuwa umeuchagua pia.

Unaruhusiwa kusindikizia na kachumbari/ au hata Salady zenu za kizungu za mahotelini

Kama ukiona hujashiba kunywa maji.

Bold

Kumbuka lengo sio kushiba bali kupunguza mwili.

Baada ya hapo ni lazima unywe tena maji ya uvugu vugu glass 4



Epukana kabisa na maswala ya juice zenye sukari nyingi

Mida ya jioni jua likishazama baada ya kazi ukirudi nyumbani, au kama utakuwa umebeba nguo za mazoezi kwenda nazo kazini. Unaweza ukatembea tena kwa nusu saa

Halafu ukamalizia na sit ups ukingoja Dinner



Ukishaoga jioni.

Huu ndio uwe mlo wako wa kufunga siku "Supu ya Samaki"

Samaki wa aina yoyote tu ile weka bakuli kubwa la kutosha.

Ila pia, hakikisha supu hiyo ni chuku chuku na haina mafuta wala viazi hata kidogo



Nikutakie siku njema na majaribio mema

Tukutane tena Day 2:

Kama kweli una nia

Hii ngoma inaenda mwezi mzima



KUMBUKA PENYE NIA PANA NJIA



No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive