Siku ya saba naiandika kwa Confidence kwakuwa haina milima wala mabonde emengi sana kama vipo ni vya kuvikabili.
Asubuhi usiache kufanya mazoezi hata iweje. Tembea dk,30 -45
Ukiwa na partner inaweza kuwa rahisi mkiwa mnasindikizana huku mnapiga story inasaidia kujisahau na kustukia muda umeisha.
Kama huna hata peke yako haina tatizo, maadam umeamua.
Ukirudi fanya sit ups nyingi kwa kadri ya uwezo wako
Kunywa maji ya moto/ vuguvugu Glass 4 kama kawaida

Yai moja la kuchemsha na maziwa Glass moja
Vipi! kuna unafuu kidogo au bado sana?

Halfu unywe Vegetable Noodle Soup pamoja na ndizi moja ya kuchemsha "Bukoba"
Sio zile ndizi za sukari.
Baada ya hapo kula matunda mengi sana ya kutosha, hata ukila ndizi mbivu pia kwa leo ni sawa tu

Jua likizama tembea dk.30-45 ukirudi fanya sit-ups ingia bafuni kuoga
Usiku ni wakati wa BBQ, wakati unangojea huku unazungumza unakunywa maji moto/vuguvugu glass 4.
Kama utachoma BBQ nyumbani ni sawa, kama utaagiza kutoka nje pia ni sawa
Ila kwa muda ule wakati unasubiri mlo unweza kunywa hayo maji
Kwasababu kuchoma nyama sio kitu rahisi sana na sio kila mtu anajua
"Hiyo mishkaki haipo kwenye diet, usiihesabu"
Unaruhusiwa kunywa glass 2 za white wine baada au wakati unakula kama ni KUKU
Au glass 2 za redwine baada au wakati unakula kama ni Beef Sausage
Manake ukifanya komeshea ukalewa kesho yake utashindwa kuamka asubuhi na hutaweza kuendelea na diet kwakuwa.
Kwanza unaweza kuwa na hang over itakayokupelekea uanze kutafuta vyakula vingine tofauti na mtiririko wa hatua hii tunayopitia.
Pia ukichelewa kuamka hutoweza kufanya mazoezi na uta skip moja ya mlo wa siku
Jiandae ya siku ya 8 ni ngumu zaidi, baada ya kuji spoil na week end
No comments:
Post a Comment