DAY 2: DIET "Kwa mlioianza jumatatu, muamke nayo kesho hii"

Kama siku ya kwanza ulitembea na kufanya sit-ups kiasi lazima siku ya pili nyama za tumbo au za miguu zitakuwa zinauma kwa kuwa hujazoea.

Ila hapo hapo zinapouma unatakiwa uendelee bila kujionea huruma mpaka zitakapoacha kuuma na uzoee kabisa



Fuatisha kutembea kwa nusu saa asubuhi, fanya sit-ups 15-20 ukishindwa fanya hata 10.

Potelea mbali kisha rudi unywe maji ya moto glass 4 kabla ya kupata breakfast.

Kaoge kabisa ila usipige mswaki kwanza:



Breakfast ya siku ya pili ni hii:

Baada ya kuoga:



Kikombe cha kahawa au chai chenye kijiko kimoja tu cha sukari

Sausage moja ya kuchemsha Beef/Chicken chaguo ni lako.

Slice 1 ya toasted brown bread na matunda mengi ya kutosha



Baada ya breakfast unaweza kupiga mswaki, ukaendelea na shughuli zako za ujenzi wa Taifa



LUNCH:

Kusema kweli kufanyia diet nyumbani saa zingine inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya vyakula

Kwa mfano leo unatakiwa ule ndizi za kuchoma, je! ni kweli kwako kutakuwa na ndizi za kuchoma mchana?? Kama inawezekana basi kheri yako.



Wakati unasubiri kuletewa chakula chako au kama unaandaa wakati unaendelea uwe unakunywa maji ya uvuguvugu mpaka zitimie glass 4



Hapo unatakiwa uchukue ndizi 1 tu ndugu, zingine waachie wenyewe. "moja tuuu!!! Okay??

Usianze kufurahia uone picha ya ndizi 5 ukadhani unatakiwa kula zote





Ndizi hizo ziendane na Kachumbari au green Salady bora iwe mboga mboga tu haijalishi ni za aina gani

Leo unaweza kula mishkaki 2 -3 ambayo sio mikubwa sana

Ila isiwe mishkaki ya Nundu

Inaweza kuwa ya Ng'ombe, Samaki au ya Kuku

Leo nafuu kidogo eti?



Mida ya jioni tembea nusu saa, ukifika home piga sit-ups 15-20.

Ukishindwa piga 10


Huu ni mwanzo ila baadae utaongeza.

Oga vizuri, pumzika, piga story huku ukiendelea kunywa maji moto/ uvugu vugu glass 4



Achana na juice ya aina yoyote iwe fresh au ya box, usiguse kabisaaa!!!!



Dinner yako ni hii, Bakuli kubwaaa la Vegetable soup

Unaweza kujazia na matunda pia mpaka saa ya kulala



Siku zote hizi usiguse Alcohol/ Pombe

Mimi pia nafanya hivyo

Siku ya ka Wine ikifika, will let you know



Usishawishike kama kweli una nia



All the Best:





No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive