.
KLABU ya Coastal Union ya Jijini hapa imepokea msaada wa vifaa vya
michezo vyenye thamani y ash 2 milioni kutoka kwa mdau wa michezo
nchini Mohamed Bawazir ikiwa ni mchango wake wa kuiwezesha kushiriki
vyema ligi kuu vodacom.
Vifaa hivyo ni jezi,mipira,beeps soks jezi za walinda mlango kwa ajili
ya wachezaji pamoja na vifaa vya uhamasishaji vya kutumiwa na
mashabiki ambavyo ni vuvuzela na tambara la hamasa.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika jana asubuhi katika hoteli ya
Tanga Beach Resort ambapo clabu ya Coastal iliwakilishwa wapenzi wake
wakiongozwa na Mwenyekiti wao,Ahmed Aurora na Makamu mwenyekiti
Steven Mguto.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Bawazir alisema lengo ni
kutoa hamasa kwa wadau wengine kujitolea kuisaidia Coastal Union
inayokabiliwa na michuano ya Ligi kuu Vodacom pamoja na kuendeleza
michezo kwa ujumla katika mkoa wa Tanga.
“Nimeamua kuongoza njia ili wadau wengine wajitokeze kusaidia kuhuisha
michezo katika mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa ikiwika katika miaka ya
nyuma kwenye michezo mbalimbali”alisema Bawazir.
Mdau huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd ya
jijini Dar es salaam,alisema kuna kila haja kwa wadau wa Tanga walioko
maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni sare jozi moja,seti mbili za sare za walinda
mlango ,soks pea 20,jezi za mazoezi jozi 30,mipira mitatu aina ya
jabulani,bendera na tambara kubwa la hamasa.
Mwenyekiti wa klabu hiyo,Aurora alimshukuru mdau huyo kwa mchango wake
mkubwa ambapo alisema vifaa hivyo vitawasaidia wachezaji pamoja
mashabiki wakati wa michuano yote inayoikabili timu hiyo.
“Bawazir amekuwa mdau wa kwanza kuisaidia klabu yetu ukiacha wadhamini
wakuu,tangu tumechaguliwa tumekuta Coastal haina vifaa wala chochote
No comments:
Post a Comment