STORY YA NILIOYAKUTA HUKU GREECE KWA KIFUPI.......IKIAMBATANA NA KA VIDEO


Hili ndio jengo la Bunge la Greece, Vurugu zote maandamano yote yakitokea break huwa ni hapa wanapiga mayoe yao wanarusha ma fataki ilimradi tu Serikali iwasikilize malalamiko yao

Naskia huku maandamano ni kitu cha kawaida na kusikia kelele za mabomu ya machozi wala sio ishu pia


Wakati nasimuliwa story hizo haijapita hata lisaa maandamano yakawasili sehemu hiyo


Mwenyeji wangu hakupata kufahamu kwa undani ni maandamano ya nini lakini inakisiwa kuwa ni wanafunzi, pengine kuna haki waliokuwa wanaililia Wanaweza kuamua tu shule ifungwe mwezi mzima


Na Askari wakiskia tu maandamano yanakuja kwakuwa huwa wanajua kilele cha maandamano huwa ni hapo wanakuwa stand by kulinda usalama na kuzuia ghasia zozote zitakazo jitokeza




Video hii nilikamata maandamano hayo kwakuwa nilikuwepo eneo la tukio Japo mpaka naondoka sikuwa nimefahamu chanzo chake ni nini


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive