NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI

Kituo cha MaishaMema Education & Training Centre ( METC ) kinatangaza nafasi za mafunzo ya kazi yatakayo wawezesha wahitimu kufanya kazi na kituo katika mradi wa Elimu ya Ujinsia na Kujitambua " MRAEUKU" .

KUHUSU MRADI ;

Mradi wa Elimu ya Ujinsia na Kujitambua ni mradi unao endeshwa na kuratibiwa na kituo ulioanzishwa kwa ajili ya kutoa elimu ya ujinsia, afya ,uzazi wa mpango na kujitambua kwa wanawake/wasichana wanao soma kwenye shule za sekondari, vyuoni, wanawake waliopo magerezani na maofisini


KUHUSU MAFUNZO:

LENGO LA MAFUNZO:

Mafunzo yamelenga katika kuwajengea wahitimu uwezo wa kutoa elimu ya ujinsia, afya na uzazi wa mpango kwa wasichana, wanawake walio katika maeneo tajwa hapo juu

MUDA WA MAFUNZO:

Mafunzo yatafanyika kwa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 05 May 2011...Na yatafanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza, itakuwa ni mafunzo ya darasani, na awamu ya pili itakuwa ni mafunzo kwa njia ya vitendo ( field training )

MAHALI YANAPOFANYIKA MAFUNZO:

Mafunzo yatafanyika katika shule ya Sekondari ya PERFECT VISION iliyopo nyuma ya UBUNGO PLAZA..

Mafunzo yatafanyika kuanzia saa 8. 30 alasiri hadi saa 12.30 za jioni...

BAADA YA KUHITIMU

Wahitimu wote wa mafunzo watafanya kazi na kituo katika Mradi wa Elimu ya Ujinsia na Kujitambua ( MRAEUKU )


SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI.

Mwombaji nafasi, lazima awe na sifa zifuatazo:

1. Lazima awe wa jinsia ya kike
2. Umri miaka 18 hadi 45.
3. Elimu kidato cha nne, sita na kuendelea..
4.Uwezo wa kuongea kwa ufasaha lugha za kiswahili na kiingereza.

FOMU ZA MAOMBI YA MAFUNZO ZINAPATIKANA KATIKA OFISI ZETU ZILIZOPO KATIKA SHULE YA SEKONDARI PERFECT VISION KWA SHILINGI ZA KITANZANIA ELFU KUMI TU ( TSHS. 10,000 )... KUANZIA SIKU YA JUMATANO,TAREHE 13/05/2011..


MUDA WA KAZI:

Jumatatu hadi Ijumaa, ofisi ipo wazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

JUMAMOSI: Ofisi ipo wazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa nane kamili za mchana.

Mwisho wa kutoa fomu za maombi ni tarehe 25/04/2011.....ILA ENDAPO IDADI YA WATU TUNAO WAHITAJI ITAKAMILIKA KABLA YA TAREHE 25/04/2011 TUTASITISHA ZOEZI LA USAJILI.

Wahi kuchukua fomu yako mapema kwani nafasi zilizopo ni chache.

KWA MAELEZO ZAIDI, PIGA SIMU : 0652458398 au 0712 224139...

TEMBELEA BLOGU YETU : http://www.maishamematanzania.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive