KUFIKA HUKU MILIMANI JUU UNAPANDA KWA TRAIN, HALAFU UNAUANGALIA MJI KWA CHINI...WATU HUENDA HUKO JUU KULA UPEPO NA KUPIGA PICHA

Hapa ni Bergen, Norway

Na hii ndio sehemu ya kupandia Train zinazowapeleka watu Mlimani.
Train hizo ziko 2, hazitumii nguvu ya umeme, ila zinatumia nguvu ya zenyewe kuvutana

Wakati Train moja inapanda, nyingine ya pili inashuka na mvutano huo ndio unapelekea zenyewe kusogea mpaka kufika mahala husika


Huko juu kuna Duka na kadhalika

Hii picha ya Sanamu inasemekana ni mfano wa Wachawi wanaoishi Norway, ambao usiku huwa wanapaa na ungo.

Zamani walikuwa wanapatikana hata hapa kwenye huu mlima tuliopiga picha
Lakini kadri miaka inavyozidi kusogea wanahamia mbali, kwakuwa binadamu wanajenga makazi yao..

Mlidhani Africa tu ndio kuna wanga, jaribuni na huku muone!!!
Imagine Ndege imekuacha unaliomba limjamaa likubebe mpaka Dar, sidhani hata kama itazidi nusu saa hujafika home
Hii sehemu niliosimama baadhi ya watu wengi huwa wanaitumia kufungia ndoa zao
Kutengeneza History tu kuwa harusi yao imefungiwa juu ya mlima

Na hayo maelezo yote nilioyatoa hapo juu sio porojo zangu binafsi.
Ndio mara yangu ya kwanza kukanyaga Norway, sasa ningeyajuaje???
Huyo jamaa hapo kulia kwangu, Mkenya flani hivi ndio alikuwa ananisimulia, yeye ndio mwenyeji aliekuwa ananizungusha.

Kama kuna vya uongo basi ni yeye.


Hassan Ngazo a.k.a Thug Life ndio Promoter wa shows za pande hizi
Kwakweli wenyeji hawa ni wakarimu

Ndani ya Train
Hili ndio lango kuu la kuingia ili upande Train ya kukupandisha mpaka kwenye Mlima
Kaa tayari kwa mengineyo meeeeeeengi, kama mnavyojua bibie mpenda picha na picha zinanipenda pia

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive