IMANI YA JICHOKeyholders, Vidani na vitu vingine vidogo vidogo vinaonekana kama mapambo
Lakini kwa Geece vina maana yake
Kama utaangalia vizuri katika picha ya hivyo vikoro koro kuna duara ambalo linaashiria picha ya Jicho

Unaweza kuwekea funguo za Nyumba au funguo za gari, Unaweza ukatundika ndani kwako au sehemu yoyote unayohisi vijicho huwa wanapitapita
Au unaweza kuvaa shingoni pia

Hivi vitu huwa wanavaa kwa imani kuwa ni protection
Inawalinda na Macho mabaya ya husda za watu
Kila duka au sehemu yoyote ya biashara ukiingia unakuta wameweka huyu mlinzi
Wengine wanaunga Vitunguu Thaumu mlangoni wananing'iniza

Ukiwa na Imani inakusaidia kukulinda na Wao Wagiriki wanaamini hivyo
Nimevinunua vitano, moja wapo ikiwa ni kidani cha shingoni nitakuwa navaa kujikinga na macho ya husda nione kama itafanya kazi

Vingine nitawagaia watu wa karibu ninaowapenda nao wajikinge na macho mabaya
Unaweza kuwa mmoja wao wa kupata hiyo zawadi usicheze mbali na mimi
Nikirudi nitakuwa naangalia nani anafaa kupewa pale Nyumbani Lounge

Hebu fikiria hilo jicho hapo juu kwenye picha likakutana na jicho baya
JICHO KWA JICHO

Hapa yanakuwa yanapambana yenyewe kwa yenyewe
Wewe umetulia tu

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive