FROGNER PARK

Hii ni Publick Park ambayo kila mtu anaruhusiwa kwenda, watalii wengi kutoka nchi mbali mbali wakifika huwa wanatembelea hapa kupata picha na kujua historia ya Park hii


Ni sehemu ambayo watu pia hufanya Picknick, Summer games na ku relax, its the Largest Park in the City


Kinachovuta zaidi ni haya masanamu yaliomo ndani mwa Park hiyo ambayo yote yako uchi hakuna hata moja lililotengenezwa likiwa limesitiriwa, na sababu sijaijuaKutokana na kila muundo wa sanamu moja, yote yanajielezea ukiyaangalia na unaweza kupata maana tofauti kutokana na hisia au dhana zako
Jide na Mwenyeji


Alie design hizi sanamu ilimchukua miezi 10
Kila sanamu moja lina uzito wa takribani tani mia moja au zaidiPichani juu ni moja ya sanamu maarufu linalojulikana kama The Angry boy.

Park hii kwa mara ya kwanza ilikuwa inamilikiwa na mtu anaitwa Hans Jacop na ndio alieigundua hii sehemu karne ya 18.
Baada ya yeye kufa ilichukuliwa na jamaa mwingine Bernt Anker miaka ya 1746 - 1805

Benjamin Wegner akaichukua 1836 na kui transform kuwa Romantic Park mwaka 1840

Na huo ukawa mwisho wa watu binafsi kuiendesha Park hiyo baada ya kuchukuliwa na Manispaa mwaka 1896 mpaka leo hii ninapo andika ujumbe huu

Park inatumika kwa michezo na maonyesho mbalimbali

Maelezo yote na mwenyeji wangu
Bijoux Amina Mbavu Karlson


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive