KILA SEHEMU KUNA VYOO VYA KULIPIA


Hapa unatumbukiza coin ndio mlango unafunguka unaingia unamaliza haja yako unatoka
TZ pia zipo za sh.mia mia ila tatizo pamoja na kulipia lakini hali ya usafi ndani huwa hairidhishi

Tatizo ni nini???????
Huwa wafanyakazi wa humo hawaipendi kazi yao?
Huwa hawalipwi mshahara mzuri?
Hakuna vitendea kazi?
Au huwa wanafanya kwa kujitolea?
Au wanalazimishwa

Manake wanavyokuwa wakali sasa

Au huenda wanaotumia vyoo hivyo huwa ni wakorofi , na kupelekewahudumu wa vyoo hivyo kuwakomesha?

Na sehemu za starehe wanawake wengine huwa wakiingia Toilet eti wanabeba toilet paper wanaweka kwenye handbags zao wanaondoka nazo.
Na wengine wanaokuja nyuma watumie nini?

Ni kwanini sasa?

Toilet paper si ni sh.300/= tu jamani


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive