Ikiwa umepita zaidi ya mwezi 1 tangu filamu ya "SHOGA" kuzuiwa na bodi ya filamu Tanzania kwa madai ya kutaka kuipitia kuona kama imekidhi vigezo na kufuata maadili ya Tanzania, mmiliki na muigizaji wa filamu hiyo Hissan Muya maarufu kwa jina la Tino ameongea na blog hii na kueleza kuwa amepata hasara zaidi ya millioni 15 za kibongo.
"Kiukweli kuzuiliwa kwa movie yangu kumeniletea matatizo sana, mipango yangu mingi imefeli na nimepata hasara zaidi ya shilingi mil.15 ambazo nilizitumia katika kufanya matangazo, na kufanya uzinduzi mikoani."
Akiizungumzia Bodi ya filamu Tino alisema-"Bodi ya filamu iache ukiritimba, kwasababu kila ninapofuatlia hawanipi majibu ya kueleweka, kila siku wananiambia nisubiri, wananiangusha sana coz kila muda unavyozidi kwenda ndivyo hasara juu yangu zinapoongezeka.
Ninachowaomba waniambie kipi kisichofaa katika filamu yangu nikiondoe ili niweze kuingiza sokoni."
Blog hii ilipojaribu kuwasiliana na katibu mkuu wa Bodi ya filamu Bi.Joyce Fisso kupitia simu ya kiganjani hakuweza kupatikana.
No comments:
Post a Comment