Lakini kwa Geece vina maana yake
Kama utaangalia vizuri katika picha ya hivyo vikoro koro kuna duara ambalo linaashiria picha ya Jicho
Au unaweza kuvaa shingoni pia
Inawalinda na Macho mabaya ya husda za watu
Kila duka au sehemu yoyote ya biashara ukiingia unakuta wameweka huyu mlinzi
Wengine wanaunga Vitunguu Thaumu mlangoni wananing'iniza
Nimevinunua vitano, moja wapo ikiwa ni kidani cha shingoni nitakuwa navaa kujikinga na macho ya husda nione kama itafanya kazi
Vingine nitawagaia watu wa karibu ninaowapenda nao wajikinge na macho mabaya
Unaweza kuwa mmoja wao wa kupata hiyo zawadi usicheze mbali na mimi
Nikirudi nitakuwa naangalia nani anafaa kupewa pale Nyumbani Lounge
Hebu fikiria hilo jicho hapo juu kwenye picha likakutana na jicho baya
JICHO KWA JICHO
Hapa yanakuwa yanapambana yenyewe kwa yenyewe
Wewe umetulia tu
No comments:
Post a Comment