NATASHA AWA MTANGAZAJI


MSANII mahiri na mwandishi wa script katika filamu nchini Tanzania Susan Lewis aka Natasha kwa sasa ni mtangazaji katika Redio Uhuru, anatangaza kipindi hiki kinaitwa "FILAMU ZETU" na kinaruka kila siku kuanzia saa 5: 45 na kumalizika saa 6:00 mchana kila siku kupitia Filamu zetu utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu filamu za hapa nyumbani.


Akiongea na blog hii Natasha ambaye ni mama mzazi wa mwigizaji Monalisa anasema kuwa anawakaribisha wasanii wa filamu kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu tasnia hii ya filamu kwa kila siku ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika kukuza sanaa hii kwani ni sekta ambayo ina uwezo wa kutoa ajira kubwa katika jamii ya Watanzania.


“Nawakaribisha wasanii na wadau wa tasnia hii ya filamu kwa hapa nyumbani, Filamu zetu ni kipindi ambacho kinaleta changamoto na kutoa mwanga kwa wasanii wote, hapa tunapata kujadili kuhusu Production, masoko ya filamu yanaendaje, na utayarishaji wa filamu kwa ujumla na mustakabali wa tasnia hii” Anasema Natasha.

SIKILIZA FILAMU ZETU REDIO UHURU KILA SIKU SAA 5: 45 HADI SAA 6:00


.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive