ASKARI WANAOSIMAMA MBELE YA BUNGE LA GREECE NI VIVUTIO MBALI NA ULINZI - WATU HUFIKA KUPIGA NAO PICHA

Wanacheza gwaride kwa muda kadhaa baada ya hapo wanaganda kwa muda wa masaa mawili hawaruhusiwi ku move wala hata kujikuna

Na wakiganda ndio watalii mnaruhusiwa kupiga nao picha
Na ukienda kupiga picha huruhusiwi kumgusa wala kumuongelesha ole wako

Hata kofia ikidondoka haruhusiwi kuiokota anagonga mtutu chini askari wa ngo ya kijani ndio anakuja kumsaidia kuweka kila kitu sawa.
Naona kama wote wanafanana kama masanamu
Ila nilikuwa natamani nimuulize kama hizi nguo zinauzwa madukani nikanunue

Ndula sasa mmmh!!! hii kiboko


Hili hapa ni kaburi la moja ya mashujaa wao ambao alifia eneo hili na akazikwa hapa hapa na imebakia kuwa kumbukumbu Picha unaruhusiwa kupiga kwa mbali huruhusiwi kugusa wala kukaribia kaburi hili





Chini kuna kipande kidogo cha Video ya Askari hao Sanamu

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive