MZEE YUSUF, JUMA NATURE KU PERFORM PAMOJA JUMAMOSI HII, TEMEKE MWEMBE YANGA KWENYE TAMASHA LA EPIQ

Meneja wa Mradi wa Epiq Nation wa kampuni ya Zantel, Deogratius Ringia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu tamasha kubwa la 'Epiq Nation' litakalofanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke ambapo wasanii Mzee Yusuf (kushoto) wa kundi la Jahazi Modern Taarab na Juma Kassim 'Sir Nature' (kulia) wa kundi la TMK Wanaume Halisi watatumbuiza.

Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim 'Sir Nature' (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu ushiriki wa kundi lake katika tamasha kubwa la Zantel Epiq Nation litakalofanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke. Kushoto ni Kiongozi wa kundi lingine litakaloshiriki la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf na Meneja wa Mradi wa Epiq Nation, Deogratius Ringia.


Kiongozi wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akieleza kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu ushiriki wa kundi lake katika tamasha kubwa la Zantel Epiq Nation litakalofanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke. Kulia ni Kiongozi wa kundi lingine litakaloshiriki la TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim 'Sir Nature' na Meneja wa Mradi wa Epiq Nation, Deogratius Ringia.


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive