MNAOMBWA MSAADA WATU WENYE MOYO WA HURUMA

Kijana Pascal Issa mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam ameomba msaada wa fedha au matibabu kwa ajili ya upasuaji wa mguu wake wa kulia wenye mifupa miwili, Kijana huyo aliyefika katika Ofisi za MO BLOG jijini Dar es Salaam.

Aidha Kijana huyo amewaomba wasamaria wema kumsaidia ili aondokane na mateso anayoyapata hususani wakati wa usiku ambapo mfupa huo wa ziada ulioanza kujitokeza tangu akiwa na umri miaka 7 mpaka sasa akiwa na miaka 24 kuendelea kukua bila matumaini ya kupata matibabu.

Kwa yoyote atakayeguswa na tatizo la kijana huyo awasiliane naye kwa namba +255657069870 au awasiliane na Meneja wa MO BLOG kwa namba +255714940992 kwa ajili ya mawasiliano zaidi.

MO BLOG inawaomba wadau wanaoweza kumsaidia hata kupata Daktari wa kumtibu kwani kutoa ni moyo na hujafa hujaumbika.Hii ni Sehemu inayoonyesha mfupa huo wa ziada unaoendelea kukua na kumsababishia maumivu makali.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive