IJUMAA TAR 22 JULY, MACHOZI BAND INASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 6, TANGU KUANZISHWA

Ni safari ndefu sana hadi kufikia sehemu ambayo wengi wanaiona kuwa ni mafanikio Kuna vikwazo, milima na mabonde lakini naamini njia ilionyooka haifunzi mengi Njia yenye drama, vilio na vicheko baadae ina hata hadithi ya kusimulia.

Kuna tulioanza nao lakini wakaishia njiani hawapo tena Kuna walioondelea mpaka leo wapo. Kuna waliotukutia njiani pia safari hawakuiweza Na kuna wapya ambao bado tunao mpaka sasa
Kuna waliopata nafasi nzuri zaidi sehemu nyingine na wakaondoka kwa amani pia tuliwatakia kila kheri
Yote hii ni safari tu

Hadithi hii tutaisimulia rasmi ndani ya Nyumba ambayo ilikuwa ni ndoto iliogeuka kuwa kweli
Nyumbani Lounge, Ijumaa tar 22 July 2011 Uongozi wa Machozi Band utatoa tuzo kwa wanamuziki na wafanyakazi wa Band yake
Kwa:
Muimbaji Bora

Mfanyakazi Bora
Mwanamuziki mwenye nidhamu

Mwanamuziki aliedumu kwa muda mrefu na Band

Mwanamuziki mwenye Talent zaidi
na nyinginezo


Trophy na fedha taslimu zitakabidhiwa kwa wahusika
Baada ya hapo kila Ijumaa na Jumapili MACHOZI BAND itakuwa inapiga Nyumbani Lounge Tumehama Mzalendo


mamama


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive