FFU wa Ngoma Africa Band kuvamia Bremen City,Ujerumani Ijumaa 16-09-2011




"Jinamizi la Bongo Dansi" LINASUMBUA ULAYA !
USO KWA USO NA WASHABIKI BREMEN CITY !
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,
wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la aina yake "AFRIKA MESSE"
mjini Bremen,nchini Ujerumani siku ya ijumaa 16-09-2011 majira ya alhasiri.
Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki katika kila kona duniani na
mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini.

Ngoma Africa band aka FFU imejikuta inapambanishwa tena uso kwa uso na washabiki
wengine katika mji wa Bremen,huko ujerumani Ughaibuni !ambapo maelfu ya washabiki
wamekaa mkao wa kula makombora ya muziki kutoka kwa bendi hiyo inayoongozwa na
kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye utajiri wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo
mwanadada Diva Bedi Beraca aka Princess Bedi Bella,pia yupo yule mcharaza solo
mahili Christian Bakotessa aka Chris-B,aka "Mshenzi wa Gitaa la solo" na wengineo,

Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na nyimbo zao "Supu ya Mawe" na
"Bongo Tambarare" zisikilize at www.ngoma-africa.com


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive