ZIARA ZA MH.MAKALLA SEHEMU MBALI MBALI


MSAADA WA MABATI 40 NA SARUJI 40 UJENZI WA KITUO CHA POLISI TURIANI.

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Turiani, Wilayani Mvomero , ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) saruji mifuko 40 na bati 40 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Turiani, ambapo ujenzi wake umekuwa ukisuasua tangu mwaka 2003 , vifaa hivyo vinathamani y ash: milioni 1.5


JENGO JIPYA LINALOENDELEA KUJENGWA.

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Polisi Turiani, Wilayani Mvomero ,akiongozwa na ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) , ujenzi wa Kituo hicho umesuasua tangu mwaka 2003 , hivyo Mbunge huyo ametoa msaada wa bati 40 na saruji mifuko 40 , vyote vikiwa na thamani y a sh: milioni 1.5

Picha ya pamoja na wadau wa miwa

Diwani wa Kata ya Mtibwa ( CHADEMA) Tusekile Mwakyoma ( aliyesimama) akisoma maswali na majibu yaliyojibiwa Bungeni kwenye kikao kilichopita na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( wapili kutoka kushoto) kuhusu kero mbalimbali wanazopata wadau wa maendeleo ya Kilimo cha miwa Mtibwa , wakati wa kikao maalumu kilichotishwa na Mbunge huyo hivi karibuni kujalidi mambo mbalimbali ili kupata maadhimo ya msingi ya kufafikisiha serikalini na Bungeni.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive