WASHINDI WA SHINDANO LA KUHESABU SHOWS ZA JAYDEE & MACHOZI BAND ZILIZOPITA

Flora Paul, kwenye kutuma Comments anatumia Binti Sayuni yuko Marekani
Ndio alikuwa wa kwanza kupatia idadi ya shindano la shows zilizopita na kupata 750,000/= Shilingi za Kitanzania

Sabah Coco ndio alikuwa mshindi wa pili, alipatia jibu sahihi pia ila Binti Sayuni comment yake ndio ilifuka ya kwanza.
Mshindi huyu wa pili alipata 250,000/= shilingi za Kitanzania

Jackrine Ngongoseke ndio mshindi wa tatu, nae alipatia jibu
Ana complimentary ya kuhudhuria shows zote popote hata akipenda kuja na Machozi Band safari atalipiwa kila kitu kwa mwaka mzima.

Sasa basi, baada ya hayo yoooote linakuja shindano lingine
This time zawadi itakuwa kubwa zaidi ya hiyo iliotoka mwanzo.

Nitatoa idadi ya show itakayo anzia Alhamis ya tar 26 May 2011
Na kuanzia hapo mtatakiwa muendeleze hesabu hadi kuja kufikia fainali ya shindano hili.

Tukijaaliwa uzima Alhamis ya tar 26 May 2011 itakuwa ni show ya 66 Tangu mwaka kuanza.

Itakapofika December 31, 2011 Tutapost picha za show yasiku hiyo na mtatakiwa kutujuza itakuwa ni ya ngapi.
Na kuanzia hivi sasa shows zote zitakuwa zina postiwa katika blog ili msikosee mahesabu

Kila heri katika shindano hili jipya.
Zawadi zitatangazwa zitakapokuwa zimekamilika. Tunaziongeza ukubwa na wingi

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive