JUMAMOSI FLANI HIVI NYUMBANI LOUNGE





Ambapo tulikuwa tumekaa tuna chill na watu mbali mbali mara zikaanza kutumwa msg, Jide hongera Jide hongera... Mara kaingia mdau wa siku nyingi Poti Poooooooooooti na mizigo miwili mkononi kabaaa

Mizigo yenyewe ndio hii

Flowers hawakusita kuikamata na kupiga nayo picha

Bahasha imeandikwa Mwimbaji Bora wa Kike, ambayo kwa kidhungu nadhani ni Best Female Vocalist. Tuzo hiyo alipewa mtu mwingine Linah wa THT.

Tuzo niliopewa mimi iliandikwa Female Artist of the Year ambayo ni Msanii Bora wa Kike wa Mwaka. Nadhani ubinaadam tu hapo umepita kama kuna fotauti na imani zitarekebishwa, kama yangu ina mpunga zaidi basi wataniongezea tu! Wink!!

Bahasha ya kwanza inanihusu nahakika ila ya pili ilioandikwa Best East African song sina hakika sana kama tunagawana na Kidum au kila mtu kapewa ya kwake???

Sina taarifa za undani, itabidi mzigo niuhifadhi nisijeanza kuutumbua mara naambiwa si zangu

Mwaka Flani hivi nakumbuka wimbo wa Anita niliofanya na Matonya ulipata kuwa Wimbo bora wa Mwaka zikatoka Trophies 2 na kila mtu akapata fungu la pesa kiasi.
Sijajua kama na kwa wimbo huu niliofanya na Kidum itakuwa hivyo au mwaka huu ni tofauti manake kila mwaka mambo huwa yanabadilika kwenye Tuzo hizi

Chef nae hakubaki nyuma




Sikuweza kufika kwenye tuzo za Kili kwakuwa sikupatiwa mwaliko, niliogopa kuzamia.
Nadhani walinisahau.........Tehe tehe tehe
Hata mwakilishi wangu yoyote pia hakuwepo ila Shabiki mmoja wapo alinipokelea na kuniletea Nyumbani Lounge

La muhimu zaidi nashukuru sana Watanzania wote mlionipigia kura, sina cha kuwalipa zaidi ya Asante
Nashukuru wote mnaoendelea kuamini kuhusu JayDee
Tuko pamoja siku zote.

Nashukuru na waandaji pia... Mbarikiwe wote


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive