MAPISHI YA CHICKEN BIRYANI

Hizi picha ni kwa kunogesha tu muonekano, unaweza pika ikawa tamu lakini si lazima itokee muonekano wake kama ambavyo picha hizi zinaonekana





Chicken Biryani

Mahitaji:

* 1 Kg Mchele Pishori (Basmati)

* 1 Kuku ikate vipande kawaida

* 1 Paket maziwa mgando

* 6 Vitunguu maji vikubwa, kata vipande round kubwa kubwa

* 1 Tablespoon Vitunguu swaumu viliotwangwa

* 1 tablespoot Tangawizi mbichi iliotwangwa



* 2 malimao

* 1 Papai bichi, menya, toa mbegu, kata vipande alafu unagrate kwenye grater, iwe chembe chembe

* Viazi mviringo kiasi (kama vikubwa, 5 vinatosha, menya uvikate half

* Nyanya ziloiva, saga kwenye blender uchuje

* tomato paste kiasi



* Mafuta ya kupikia, kiasi

* Chumvi Kiasi

* Cinnamon

* Pilipi8li Manga kiasi

* Karafuu kiasi

* Hiliki kiasi * Zafarani (saffron) kiasi (iloweke katika maji ya moto nusu glass)

Jinsi ya kupika



*Weka ndani ya blender Tangawizi, papai ilosagwa na kitunguu swaumu na maziwa mgando uvisage mpaka view mchanganyiko mzito. Weka pembeni

* Osha kuku kisha ipake chumvi ukamulie malimao, mwagia mchanganyiko wa papai na tangawizi na vitunguu swaumu kasha weak jikoni uchemshe mpaka iive iwe laini (kama kuku ya kienyeji. ikiwa kuku ya kizungu usiichemshe sana itavurugika)

* Saga spices zako zote pamoja kisha uweke kwenye kuku ikiwa inachemka



* Weka nyanya iliosagwa kwenye blender na ile ya paste kwenye kuku inayochemka, ukoroge ichanganyike kwenye nyama

* Menya vitunguu maji uvioshe uvikate. Weka sufuria jikoni uweke mafuta yachemke. Weka vitunguu maji ukaange mpaka viwe golden brown. Viipue uchuje mafuta uviweke pembeni vipoe.



* Menya viazi mviringo uvikaange kwenye mafuta mpaka viive, ipua weak pembeni vipoe

* Kama kuku imeiva, isikauke iwe na rojo, chuku vitunguu uliokaanga uvimimine kwenye kuku, na viazi pia, changanya, acha ichemke kiasi halafu ipua weak pembeni tayati kwa kuliwa.

* Weka sufuria jikoni utie maji na chumvi, yakichemka tia mchele na mafuta. Pika kama wali kawaida unavyopikwa. Wali ukishaiva nyunyizia yale maji ya zafarani huku unageuza ili rangi isamba. Kama huna zafarani basi tumia food coloring ya orange. Funikia na uweke moto mdogo sana mpaka wali ukauke vizuri (hii ni kama haupalii na mkaa kwa juu.

NB: Kama utapenda unaweza kuweka zabibu kavu pia wakati unaweka mchele kwenye maji ya moto zinaivia humo



Recipe na: Sabah Coco

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive