JINSI YA KUPIKA UYOGA

Humo ndani kuna uyoga wa aina nyingi sana na tuliuchanganya wote kwa pamoja nikaupika kwa nyanya na vitunguu na mafuta, majina ya uyoga huo ni haya hapa, Ushikoa, Unkese, uyungwe, Kaujogoo, Wikundi kundi, Ndevu za Babu na Untyelele. Wote huu upo humo, mtamu sana.

UYOGA FRESH, umechumwa shambani, huu ni ule unaoota wenyewe mashambani na sio wa kupandikizwa kama wa mijini.

Uyoga ukisafishwahasa kutolewa udongo ktk mashina na kukatwa katwa vipande vya size ndogo

Unausafisha uyoga vizuri na maji ili mchanga na udongo usiwepo

Unakaanga vitunguu na nyanya, vikiiva na kulainika unaweka uyoga wako ulio msafi, unageuza geuza vichanganyikane, unaweka chumvi
Ukiiva unakua rangi hii, pia kuna wanaopika bila nyaya, ni namna mtu apendavyo, unakula kwa ugali, wali, viazi n.k


Recipe hii imetumwa kutoka TABORA

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive