TANZANIA MITINDO HOUSE INATOA NAFASI 10 ZA MWALIKO WA CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO WA KITUO HICHO - NI KWA WADAU 10 WA BLOG YA LADY JAYDEE



TANZANIA MITINDO HOUSE INAPENDA KUWAALIKA WADAU KUMI WA BLOG ZA 8020FASHIONS,LADYJAYDEE, ISSAMICHUZI NA DINA MARIOS

KATIKA KUELEKEA SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI, TMH IMEANDAA CHAKULA CHA MCHANA NA KUONYESHA UPENDO KWA WATOTO YATIMA, INAWASHIRIKISHA WADAU WA BLOGS AMBAZO ZINATOA SANA SUPPORT KWAO .

TMH VALENTINE CELEBRATION – WATOTO FUN DAY. ITAFANYIKA TAREHE 13 MWEZI WA PILI 2011 VIWANJA VYA TMH FUN CENTRE KIGAMBONI

KUANZIA SA NNE ASUBUHI MPAKA SA KUMI JIONI

WATOTO FUN DAY INADHAMINIWA NA KCI, IKU LAZARO NA LONGMAN





JIDE:

Kwa Upande wa Blog hii ya JayDee......ningependa watu kumi wa kwanza watakaotuma comments kwa open ID, waniandikie na e-mail pia ili tuwasiliane tuweze kushiriki pamoja katika hafla hii ya kujumuika na kuwafariji watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu......

Sio mbaya watakaopata nafasi hiyo wakija pia na zawadi au vitu mbali mbali kwaajili ya kuwapa watoto au kuchangia, vitu kama Madaftari, Unga, Sabuni, Sukari, Mafuta au chochote kidogo kwa uwezo wako.

Ikishindikana kuwapata kwa njia hii, nitajaribu kuchagua wadau wa siku nyingi ninaoamini wataweza kushiriki kwa moyo. Ila ningependa na wengine wajumuike ambao sio walewale wa siku zote





No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive