FRONTLINE MANAGEMENT YAINGIA UBIA NA KAMPUNI KUBWA


Heri ya mwaka mpya!

Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima na kwamba mnaendelea vizuri na kazi na majukumu mbalimbali yanayowakabili.

Frontline Management inayofuraha kuwatangazia kuwa tumeingia ubia na kampuni kubwa ya kimataifa ya mahusiano ya jamii (Public Relations)

Ijulikanayo kama Porter Novelli.

Porter Novelli, kampuni iliyoanzishwa mwaka 1972 huko Washington Marekani, ina jumla ya ofisi 100 kwenye nchi zaidi ya 75.

Ubia huu utatuwezesha kuwahudumia wateja wetu kwa ubora zaidi, pamoja na kusaidia kujenga na kuimarisha huduma za mahusiano ya jamii nchini.

Kampuni ya Frontline imeteuliwa na Porter Novelli kwa sababu ya uhodari wa uchapakazi wake uliojidhihirisha kwenye miaka miwili ambayo Frontline imekuwa ikifanya kazi.

Nimeambatanisha press release yenye habari kamili, na picha kadhaa mnazoweza kutumia mojawapo ikiwa ni ya Global CEO wa Porter Novelli Mr. Gary Stockman akimpa mkono wa pongezi MD wa Frontline Ms. Irene Kiwia na kumkaribisha rasmi kwenye mtandao huo wa kimataifa.

Habari hii inaonyesha ni jinsi gani kwenye nia kuna njia, kwani kampuni ya Frontline imeweza kukua ndani ya miaka miwili na kujiunga na kampuni kubwa ya kimataifa kama Porter Novelli.

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu wa kila siku.

Wenu katika ujenzi wa Taifa,

KIWIA, Irene E.

Managing Director

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive