TOVUTI MPYA INAYOHUSU MASUALA YA AFYA


Tovuti ya Afya

www.tanzmed.com

TanzMed ni mjumuiko wa wataalamu wa fani mbalimbali za Afya wa kitanzania ambao wamejitoa katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania na Afrika kwa ujumla inafaidika kwa kupata habari na ushauri juu ya masuala ya afya yanayozunguka jamii hizo. Lengo kuu la tovuti hii ni kuleta mwamko kwa Watanzania katika kufahamu umuhimu wa kuwa na Afya bora kwa njia ya mawasilianoya mtandao. TanzMED imedhamiria kuwa chanzo kimojawapo cha habari, elimu, ushauri na mengi mengineyo yahusuyo afya.
Maana ya TanzMed

TanzMED ni muungano wa maneno mawili, “Tanz” ambalo linawakilisha Tanzania na “MED” ambalo linawakilisha Medicine.

TanzMED Forums - forum.tanzmed.com

TanzMED Forums

TanzMED Forums ni jukwaa linalopatikana ndani ya tovuti ya tanzMED ambalo kusudio na lengo lake ni kuwawezesha wanajamii kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu afya kwa ujumla.

Ndani ya TanzMED Forums kuna majukwaa kama,afya ya akina mama na watoto,magonjwa,lishe na madawa,Mahusiano vilevile ushauri nasaa.

Hivyo basi TanzMED Forums ni suluhisho la maswali yote ya afya yako.

Powerd by AfroIT Group

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive