MPANGO WA KUIKUZA FAMILIA YA BINTIMACHOZIKwa takribani miaka miwili na zaidi iliopita Kupitia blog hii, hii nilifanikiwa kukutana na watu ambao baadae baadhi yao wamekuwa karibu sana na tumekuwa tukishirikiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya kijamii, ikiwemo Misiba, Harusi na hata katika furaha zinginezo.


Ni jambo la busara kubadilishana mawazo na kuishi kama Familia
Watu hao sikuwa nawajua kwa sura ila walikuwa wanachangia tu maoni humu ktk blog
Nikaandaa shughuli ya kuwakaribisha Nyumbani, tukala chakula kwa pamoja, tukacheka, tukaunda undugu na mpaka leo tunajiona kama Familia

Watu hao ni:
ESTER ULAYA, MAGGIE, FARAJI, CUTE SMILE, SAB, CHRISTINE, SOPHIA, IMA "The Designer", KAI, PM, na SHANGWE al-maarufu kama DISMINDER


Inawezekana ki ubinadamu kuna ambao nimewasahau mtanisaidia kuwakumbusha.

Nia na dhumuni la kuandika barua hii, Ni kuwataarifu kuwa nina mpango wa kuongeza watu wengine niwajumuishe katika Familia hii kama watapenda kushirikiana nasi.
Kwani ningependa siku moja Familia iwe na watu zaidi hata ya Alfu moja.

Mwaka huu mwishoni, Mwezi December nategemea kuandaa sherehe ambayo nitaalika wanafamilia wapya 50, ila ni wale tu wanaochangia maoni yao kwa Open ID.
Kwakuwa hao ndio inakuwa rahisi kujua ni kina nani, anony inakuwa ngumu kidogo.

Na kwa sasa nimefanikiwa kupata list ya majina 15 tu, ila mpaka December na hakika idadi inaweza kuwa imefikia 50
Ambapo tutangana na wana Familia wa zamani kuufunga mwaka na kufahamiana ili tushirikiane katika mambo yalio ya msingi kujijenga sisi na jamii inayotuzunguka.

Nitatangaza tarehe ya shughuli baada ya kupata idadi kamili ya wanafamilia wapya na wa zamani........Chakula, Vinywaji na Sheesha vyote vimelipiwa.
Mtatakiwa kuleta furaha zenu tu ili kuikamilisha siku....Shughuli itafanyika NYUMBANI LOUNGE

Baadhi ya majina mapya ambayo nimeona yatafaa kujumuishwa katika Familia ni pamoja na:

1. Simon Kituturu
2. Mama Siyabonga
3. Kai Rooney
4. Jide's Sescret Admirer
5. Monica
6. Eunice
7. Nesha (Ngeze)
8. Bob_Dash
9. Sofi
10. Edna
11. Flower
12. lisa
13. happy
14. Kinyerezi
15. Kadadaa
16. Mdau essien


Asanteni kwa ushirikiano wenu na kuleta changamoto, cant wait to see you pipo.
Tukishakutana inabidi tupeane majina ya ukweli na sio nicknames tena.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive