IBILISI MMOJA MBEYA AMUUA BINADAMU ANAEDAIWA KUWA ALIKUWA NI MKEWE

Mwenyezi Mungu amsamehe na ampe moyo wa kurudi nyuma kukumbuka, kujutia na kutubu madhambi yake.

Hapa mtuhumiwa akionyesha sehemu aliomyweshea sumu mkewe

Dada wa marehemu akipewa pole baada ya machungu ya kuondokewa na ndugu yake


Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.

Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Loading...

Blog Archive