MAISHA UPANDE WA PILI WA SARAFU


Vipi kama unazaliwa huku, unakulia huku na unasoma katika maisha haya ya huku, unaishi huku mpaka unazeekea huku?
Ni bora kuliko kuja mjini?

Ila naona sivyo, labda ndio maana kila mtu anakimbilia mjini
Ila ingekuwa poa kama kungekuwa na elimu na mambo kama ya mjini katika mazingira haya halafu hao wanaoishi huku wapajenge kwao pawe kama mjini ili wasikimbilie mijini

Huku hakuna hali ya msongamano kama mjini
Hakuna joto kama mjini, Ni baiskeli tu tena wala sio nyi nyingi kama magari ya mjini
Ajali si mara kwa mara labda iwe ya kuumwa na nyoka shambani au kuanguka toka juu ya mti
Au kutumbukia kisimani wakati unateka maji

Huhitaji steelwire kusugulia hizo sufuria zinazoonekana zinang'aa hapo juu
Unahitaji mchanga laini tu ambao huundwa kama kichuguu na wadudu wanaojenga maskani yao pembezoni mwa nyumba wanaojulikana kama Fukufuku

Hapo kilichogharimu ni hayo masufuria tu
Ila hiyo miti iliotumika kutengenezea chaga ni bure

Huhitaji kununua kuku toka kwa mtu manake unaweza ukafuga mwenyewe na mgeni akija unamchinjia Kuku wa Kienyeji, wala hilo sio jambo la anasa.
Sio hatari kulala kwenye nyumba ambayo haina madirisha madhubuti kwa kijijini


Lakini katika maisha ya kila siku pia huwezi kula Kuku Daily, itakuwa ni Ugali mkubwa, mboga ndogo



Ila ukitembea kilomita kadhaa huwezi kuacha kukutana na wanyama kama Pundamilia na wengineo wengi

Huku panaitwa BUNDA, ni mkoa wa MARA...Mkoa ambao rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitokea na Lady JayDee pia asili yake na ya wazazi wake ni huku. Japo hakuzaliwa mkoani Mara

Huu ni mwanzo wa story ambayo ukipenda unaruhusiwa kuifuatilia, tukijaaliwa uhai mwisho wake utakuwa mzuri.......Ni story ya kujenga.
Pnapomajaaliwa tukutane ukurasa wa pili

Picha zote kwa hisani ya:
Captain G. Habash
Alietembelea Bunda mwezi July


No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive