Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Babu Sikare maarufu kwa jina la Albino Fulani ambae pia ni CEO wa Afrobino akiwa katika kituo cha Malezi ya watu wenye Ulemavu wa ngozi cha Shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga ambako alitembelea na kutoa misaada ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Sunscreen), Kofia na Mianvuli.
Akiongea katika shule ya msingi Buhangija mkoani Shinyanga Sikare aliweza kuzungumza na mwanafunzi Kabula Nkalango ambaye alinusurika kuuawa katika mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kukatwa mkono wake wa kulia na kumkabidhi msaada huo kwa niaba ya walemavu wengine.
Bwana Sikare alisema kuwa maalbino wasiojiweza wanaweza kuishi miaka mingi wakiwezeshwa kwakupewa misaada ya kuzuia cancer ya ngozi. Aliwashukuru watu wote walio unga mkono "Save Albino Concert" iliyofanyika hivi karibuni huko Houston, TX. Pia aliwashukuru wadhamini wao ESM Travel ya Chicago Usa, Boombastic Sound ya Houston TX, Studio Elements ya Houston TX na Pillarsis ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment