captain kishen savani congratulates imran Hirjee on a gud run



Timu ya kriketi ya Hennessy Hitters ya jijini, imeibuka kidedea baada ya kuishinda timu ya ‘Not So Hot Chilies’ kwa magoli 135 kwa 89 katika viwanja vya ndani vya Funkys Orbit Masaki


Katika mchezo huo kabambe wa ufunguzi, uliweza kutiwa chachu ya mabadiliko makubwa na Kevin Patel wa Hennessy Hitters ambae alionyesha umahiri mkubwa uwanjani hapo, pamoja na ndugu wawili Imran na Nadir Hirji wa timu hiyo.


Akizungumza baada ya mchezo, nahodha wa Hennesy Hitters, Kishen Savani amesema, amefurahishwa sana na ushindi huo kwa kuwa walikuwa wakiutarajia toka awali, “umekuwa ni mwanzo mzuri tulioutarajia,kwa kuwa tulikuwa tumejiandaa vilivyo, kwa kweli nimefurahi sana, na wapinzani wetu wengine wajiandae tu kwa vipigo mfululizo” alisema nahodha huyo.


Hennessy ambayo inaamini, na kuwa mstari wa mbele katika kuinua vipaji na ubunifu katika nyanja mbalimbali za kimaisha, inajivunia sana kuwa mdhamini wa Hennessy Hitters ambayo itaingia tena katika viwanja vilevile vya Funkys Orbit tarehe tatu ya mwezi huu, saa moja kasorobo kwa mpambano mwingine kabambe na timu ya Cocacola.



No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive