VINCENT BONIFACE
Dar es Salaam ni moja ya jiji lenye mkusanyiko mkubwa wa watu wenye ulemavu wanaokusanyika katika makutano tofauti ya barabara za jijini kuomba msaada kwa wapita njia kwa madhumuni ya kujipatia riziki.
Vincent Boniface ambaye ni mlemavu anayejitafutia riziki katika junction ya Morocco jijini Dar es Salaam alifanya mahojianona blog hii kuelezea nini kilimsibu mpaka kufikia hali aliyonayo sasa.
“Nilizaliwa miaka 36 iliyopita mkoani Kigoma nikiwa mzima wa afya lakini baada ya kipindi kifupi nikaugua ugonjwa Polio uliopelekea upungufu wa madini fulani katika mifupa yangu, kutokana upungufu wa madini hayo nilipotimiza umri wa miezi sita nikaanza kuvunjikavunjika mifupa na kupelekea kutokea kwa hali hii niliyonayo hivi sasa.”
Qn:Dar es Salaam ulikuja lini na kwa madhumuni gani?
“Dar es Salaam nilikuja mwanzoni mwa miaka ya tisini kwa madhumuni ya kutafuta tiba ya ugonjwa wangu lakini kutokana kutokuwa na uwezo wa kifedha na kuchelewa kupata huduma za kitabibu madhara yakazidi kuwa makubwa sana.”
Qn:Ilikuwaje mpaka ukafikia kuomba barabarani?
“Nilipofika Dar nilifikia kwa ndugu yangu ambaye hali yake kiuchumi haikuwa nzuri hivyo ili kumpunguzia mzigo nikaamua na mimi kujitafutia kwa kwenda kuomba barabarani.”
Qn:Kwa sasa unaishi wapi, na nani?
“Sasa hivi naishi na rafiki yangu ambaye huwa ananisaidia katika kuniendesha kwenye baiskeli yangu, na kutokana na kukosa samani za kuniwezesha kupanga chumba hivyo tumepanga katika gesti ya Shimbo iliyopo maeneo ya Kinondoni ambayo tunalipa shilingi 7000 kwa siku.”
Qn:Ni matatizo gani unakumbana nayo katika kazi yako.
“Matatizo ni mengi lakini kikubwa ni kwamba watu wengine wana dharau sana, na pili barabarani kiukweli sio sehemu yenye usalama hivyo muda mwingine Napata shida sana.”
Qn:Je akitokea mtu anayetaka kukusaidia,ungependa akufanyie nini na utakuwa tayari kuacha kuomba barabarani?
“Kiukweli nitafurahi sana kama akitokea mtu wa kunisaidia, na ningependa kufunguliwa biashara ambayo itaweza kuniingizia kipato cha kuniwezesha kupambana vizuri na maisha na pia nitakuwa tayari kuachana na kazi ya kuomba barabarani.”
Qn:Kila binadamu wa kawaida huwa na starehe yake, je Vincet unapenda starhe gani?
“Kiukweli mi starehe yangu kubwa ni muziki, na mahali ambapo napenda kwenda ni Mango Garden kila alhamisi kuangalia muziki wa taarab wa kundi la Jahazi Modern Taarab.”
No comments:
Post a Comment