Wafanyabiashara wakubwa 15 wa Dar Es Salaam wameungana pamoja kushiriki katika ligi ya mashindano ya ndani ya kriketi yatakayoanza mwishoni mwa mwezi wa kwanza. Wananchi wamealikwa kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Hennesy Hitters inayoongozwa na Kepteni Kishen Savani, katika mechi yao ya ufunguzi itakyofanyika Jumatatu ya tarehe 31 mwezi huu, saa tatu usiku, viwanja vya Funkys Orbit (Masaki)
Kwa falsafa ya Hennessy (LVMH), ambao wanaamini katika ubunifu na suala zima ugunduzi katika maisha , na hiyo ndio sababu ya Hennessy kushiriki na kutoa udhamini huo.
“timu yetu imeundwa na marafiki wa karibu ambao ni wachezaji wa mchezo huu enzi ya ujana wetu” alisema nahodha Savani, “ tumekuwa tukijifua vilivyo kwa muda wa wiki chache zilizopita, na kwa sasa tuna timu imara mbapo tunaamini ushindi katika mechi hii ya ufunguzi”.
Timu ya Hennessy Hitters inaundwa na kundi la wafanyabiashara wafuatao: Kisheni Savani (Kepteni wa timu), Chintui Patel (Kepteni msaidizi), Kevin Patel, Nishit Kanabar, Imran Hirji, Heri Bomani, Nadir Hirji, Nitesh Patel, Prahld Nathwani, Rupesh Kanabar, Situ Ramji, Akash Patel, Pullen Manek, Anand Patel na Gopal Patel.
“kwa hadhi tuliopewa na jamii, tunaamini huu ni wakati wa sisi na jamii kuwa pamoja katika mafanikio yetu na kwa kila mmoja wetu “-LVMH(Louis Vuitton. Moet Hennessy)
Mechi zinazofuata zitachezwa tarehe 31 mwezi huu, tarehe 3, 8, 10, na tarehe 18 katika mwezi wa pili.
Kwasasa Hennessy (LVMH) ni kingozi wa Cognac , ambayo inauza chupa zaidi ya milioni 50 duniani kote.
Kwa maelezo zaidi, tembelea http://www.lvmh.com
No comments:
Post a Comment