TANZANIA MITINDO HOUSE INAPENDA KUWAALIKA WADAU KUMI WA BLOG ZA 8020FASHIONS,LADYJAYDEE, ISSAMICHUZI NA DINA MARIOS
KATIKA KUELEKEA SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI, TMH IMEANDAA CHAKULA CHA MCHANA NA KUONYESHA UPENDO KWA WATOTO YATIMA, INAWASHIRIKISHA WADAU WA BLOGS AMBAZO ZINATOA SANA SUPPORT KWAO .
TMH VALENTINE CELEBRATION – WATOTO FUN DAY. ITAFANYIKA TAREHE 13 MWEZI WA PILI 2011 VIWANJA VYA TMH FUN CENTRE KIGAMBONI
KUANZIA SA NNE ASUBUHI MPAKA SA KUMI JIONI
WATOTO FUN DAY INADHAMINIWA NA KCI, IKU LAZARO NA LONGMAN
JIDE:
Kwa Upande wa Blog hii ya JayDee......ningependa watu kumi wa kwanza watakaotuma comments kwa open ID, waniandikie na e-mail pia ili tuwasiliane tuweze kushiriki pamoja katika hafla hii ya kujumuika na kuwafariji watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu......
Sio mbaya watakaopata nafasi hiyo wakija pia na zawadi au vitu mbali mbali kwaajili ya kuwapa watoto au kuchangia, vitu kama Madaftari, Unga, Sabuni, Sukari, Mafuta au chochote kidogo kwa uwezo wako.
Ikishindikana kuwapata kwa njia hii, nitajaribu kuchagua wadau wa siku nyingi ninaoamini wataweza kushiriki kwa moyo. Ila ningependa na wengine wajumuike ambao sio walewale wa siku zote
No comments:
Post a Comment