IPP CARES FOR YOU

CEO wa IPP MEDIA Bw. Reginald Mengi, kila mwaka hufanya hafla ya chakula cha mchana kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali hapa nchini.
Lengo ni kuwajumuisha pamoja, kufurahi pamoja na kudumisha usawa wa binaadamu.

Katika kunogesha hafla hizo wasanii mbali mbali wa muziki hapa nchini hualikwa pia ili kuwapa nafasi wahusika wa hafla hiyo ambao huwa hawapati fursa mara kwa mara kuwaona wanamuziki wanaowapenda.

Baadhi ya wafanyakazi wa IPP MEDIA akiwemo Mkurugenzi Bi.Joyce Muhavile katika picha ya pamoja na JayDee

Mr. Diamond aliteka show vibaya sana, ndio wakati wake huu jamani muacheni kijana a shine



Watangazaji wa radio mbalimbali zinazomilikiwa na IPP MEDIA


Mwana F.A na A.Y walikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokonga mioyo ya wahudhuriaji pamoja na watoto wadogo ambao ndio wanaoujua sana muziki wa kizazi kipya kuliko hata wazazi wao



Ali Kiba alipopanda nadhani watoto walishangiliaaaa!!!!walianza ku imagine kuwa wamegusana na R.KELLY vile..
Chezeaaa Kiba, alikuwa msafiiiiiiii unaogopa hata kumgusa usije ukamchafulia shati lake jeupe bure

KUTOA NI MOYO SIO UTAJIRI

No comments:

Post a Comment

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive