YA LEO

YALIOJIRI WEEK END......




The Arcade mambo yalikuwa kama hivi

Waliokuja kwa mbwembwe wengine walirudi na huzuni zao nyumbani

Walioweza kustahamili waliendelea kula burudani ya Machozi Band baada ya match


Hii ilikuwa ni umamosi ya tarehe 28 May 2011

Michezo mingine pia ilikuwepo mbali na kuangalia mpira


Jerome Heineken ndio alikuwa host wa hiyo kitu



Red Carpet na watu walipata nafasi ya kupiga picha hapo


Ni usiku wa Heineken ndani ya Arcade ambapo Man U walilala Doro

NYUMBANI LOUNGE JUMAPILI.


Mwanangema & Mama Kibunju

Photo session ilianzia hapa watu huwa hawachokagi kuomba picha kwa Hasheem kiiiiiiila siku

Wahudumu nao wanaacha kazi wanakimbilia picha




Muendelezo wa mahesabu ya shows




Steve Nyerere kazini aliimba siku hiyo

Sanya Ilikuwa Alhamis Nyumbani Lounge
Ijumaa MZALENDO
Jumamosi Arcade
Jumapili Nyumbani Lounge

Picha za Alhamis na Ijumaa hazikuweza kupatikana kwakuwa hapakuwa na mpiga picha wa kueleweka

RATIBA YA SANYA SANYA WEEK END HII

Alhamis ya Tar 26 May 2011. Machozi Band itakuwepo Nyumbani Lounge

Ijumaa ya tar 27 May LADY JAYDEE na Machozi Band watakuwepo Mzalendo Pub
Beba Shangwe mfukoni na raha kiunoni, hakuna kukaa chini kwenye viti

Jumamosi Lady JayDee na Machozi Band watakuwepo The Arcade - Mikocheni kujumuika na kufurahia pamoja na wapenzi wa football baada ya Match ya Fainali ya UEFA Champions League kati ya Manchester United na Barcelona

Na Jumapili Machozi Band itamalizia Nyumbani Lounge
Mpango mzima hapa ni kuvalia tu vizuri
Flowers piga kiatu chako matata kionekane
Friends na wadau baneni kwa pembeni muangalie show

See you there

YANAYO ENDELEA NYAMONGO


Ndugu zangu,

PICHA ya jeneza lililotelekezwa barabarani imeongea zaidi ya maneno milioni moja. Kwa Watanzania, imetutia simanzi, imetutoa machozi. Ndani ya jeneza hilo pichani kuna mwili wa marehemu Emmanuel Magige iliyotelekezwa kijijini Nyakunguru, Tarime. Emmanuel Magige hakuwa jambazi. Ni Mtanzania mwenzetu mwanakijiji wa kawaida. Aliyetelekezwa si Magige tu, kuna maiti nyingine tatu.


Mauaji ya Nyamonngo yanatukumbusha Arusha, yanatukumbusha Mbarali. Yanatutia hofu mpya pia. Hatujui kesho yatafanyika wapi.Kupunguza aibu hii ni kwa wote waliohusika na mauaji haya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Jeneza la Emmanuel Magige lililotelekezwa barabarani ni kielelezo cha mahali tulipofikia. Kuna chuki inajengeka. Na katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania. Tusifike mahali tukachochea machafuko makubwa ya kijamii. Wanasiasa wana jukumu la kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.

Na tuyalaani vikali mauaji ya Nyamongo. Tusipoyalaani nasi tutalaaniwa. Na Mungu huyu anatupenda Watanzania, kuna tunachoonyeshwa. Na tuzisome kwa makini alama hizi za nyakati. Na Miungu yetu, mizimu ya mababu zetu, inatupenda pia. Walikolala mababu zetu, nao wanaturajia tulaani kitendo hiki, maana, hata katika mila na desturi zetu, Waafrika hatutelekezi maiti zetu. Tunazizika.

Ndio, kwa jadi yetu, Waafrika tunahesabu wafu wetu, tunawatambua kwa majina, tunawaombea kwa imani zetu. Ndio, tunawazika wafu wetu. Kwa heshima zote.
Kwa desturi, Watanzania hatupendi kuwa katika hali ya kudharauliwa na kutothaminiwa kwa utu wetu tukiwa hai. Na kamwe, tusikubali Watanzania wenzetu wasithaminiwe wakiwa katika hali ya umauti. Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid
Iringa,
Alhamisi, Mei 26, 2011

UTAKAVYOKUTANA NAVYO NYUMBANI LOUNGE






Chaguo ni lako
Tuko wazi Monday - Monday
Kuanzia saa 6Mchana mpaka Usiku mwingi

82Ada Estate, Tranic Plaza
Kinondoni Dar es Salaam
Karibu na BestBite

WASHINDI WA SHINDANO LA KUHESABU SHOWS ZA JAYDEE & MACHOZI BAND ZILIZOPITA

Flora Paul, kwenye kutuma Comments anatumia Binti Sayuni yuko Marekani
Ndio alikuwa wa kwanza kupatia idadi ya shindano la shows zilizopita na kupata 750,000/= Shilingi za Kitanzania

Sabah Coco ndio alikuwa mshindi wa pili, alipatia jibu sahihi pia ila Binti Sayuni comment yake ndio ilifuka ya kwanza.
Mshindi huyu wa pili alipata 250,000/= shilingi za Kitanzania

Jackrine Ngongoseke ndio mshindi wa tatu, nae alipatia jibu
Ana complimentary ya kuhudhuria shows zote popote hata akipenda kuja na Machozi Band safari atalipiwa kila kitu kwa mwaka mzima.

Sasa basi, baada ya hayo yoooote linakuja shindano lingine
This time zawadi itakuwa kubwa zaidi ya hiyo iliotoka mwanzo.

Nitatoa idadi ya show itakayo anzia Alhamis ya tar 26 May 2011
Na kuanzia hapo mtatakiwa muendeleze hesabu hadi kuja kufikia fainali ya shindano hili.

Tukijaaliwa uzima Alhamis ya tar 26 May 2011 itakuwa ni show ya 66 Tangu mwaka kuanza.

Itakapofika December 31, 2011 Tutapost picha za show yasiku hiyo na mtatakiwa kutujuza itakuwa ni ya ngapi.
Na kuanzia hivi sasa shows zote zitakuwa zina postiwa katika blog ili msikosee mahesabu

Kila heri katika shindano hili jipya.
Zawadi zitatangazwa zitakapokuwa zimekamilika. Tunaziongeza ukubwa na wingi

PIC OF THE DAY..

WIMBO MPYA WA NURU "The Light" na Mr.Chocolate Flava

HABARI NJEMA KWA WASANII CHIPUKIZI WA KIZAZI KIPYA

HABARI NJEMA SANA KWA WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA..

Je wewe ni msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya?
Umerekodi wimbo wako lakini haupigwi redioni?
Unaamini wimbo wako ni mzuri na unaweza kuwakamata mashabiki?

Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako, Kampuni ya PROMO MEDIA ENTERTAINMENT ni waandaaji wa kipindi kipya cha redio
“CLUB BONGO “. Kipindi kitaanza kurushwa rasmi tarehe 04/06/2011 kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne kamili usiku kupitia PASSION FM. Na kitakuwa kikikujia hewani kila siku ya jumamosi saa tatu hadi saa nne kamili usiku.

Kipindi hiki ni kwa ajili ya kupromoti nyimbo za wasanii chipukizi wenye nyimbo nzuri lakini wameshidwa kuzipeleka redioni..

Leta wimbo wako katika ofisi zetu, Ofisi zetu zipo nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA BUILDING…

Leta wimbo wako mapema, wasanii watakao leta nyimbo zao mapema ndio watakao pata nafasi ya kwanza kupigiwa nyimbo zao redioni…

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba
0652458398 AU 0788363058..

Kwa walioko nje ya Dar es salaam, Tuma kazi yako kwenda kwa:
Managing Director,
PROMO MEDIA ENTERTAINMENT
P.O.Box 35967
Dar es salaam.

PROMO MEDIA ENTERTATINMENT, MKOMBOZI WA WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA.

ZIARA ZA MH.MAKALLA SEHEMU MBALI MBALI


MSAADA WA MABATI 40 NA SARUJI 40 UJENZI WA KITUO CHA POLISI TURIANI.

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Turiani, Wilayani Mvomero , ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) saruji mifuko 40 na bati 40 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Turiani, ambapo ujenzi wake umekuwa ukisuasua tangu mwaka 2003 , vifaa hivyo vinathamani y ash: milioni 1.5


JENGO JIPYA LINALOENDELEA KUJENGWA.

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Polisi Turiani, Wilayani Mvomero ,akiongozwa na ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) , ujenzi wa Kituo hicho umesuasua tangu mwaka 2003 , hivyo Mbunge huyo ametoa msaada wa bati 40 na saruji mifuko 40 , vyote vikiwa na thamani y a sh: milioni 1.5

Picha ya pamoja na wadau wa miwa

Diwani wa Kata ya Mtibwa ( CHADEMA) Tusekile Mwakyoma ( aliyesimama) akisoma maswali na majibu yaliyojibiwa Bungeni kwenye kikao kilichopita na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( wapili kutoka kushoto) kuhusu kero mbalimbali wanazopata wadau wa maendeleo ya Kilimo cha miwa Mtibwa , wakati wa kikao maalumu kilichotishwa na Mbunge huyo hivi karibuni kujalidi mambo mbalimbali ili kupata maadhimo ya msingi ya kufafikisiha serikalini na Bungeni.

MSANII MPYA C-SIR



Mambo vipi,
Nachkua nafasi hii kukushkuru sana kwa support unayoendelea kutupatia kiukweli bila mchango wako hatuwezi fika popote.

Sisi kama TETEMESHA RECORDZ tumejiwekea malengo ya kuwa tunajaribu kutafuta wasanii wachanga kabisa lakini wenye vipaji na kuwapika kisha kuwatambulisha katika music industry hapa TZ.

Tulianza na HUSSEIN MACHOZI, akafuata SAJNA na sasa ni zamu ya msanii mwingine mpya C-SIR MADINI kutoka Mwanza.

Huyu tunaemtambulisha sasa jina lake kamili ni PETER MPONEJA, na jina lake lingine la nyumbani ni MASISA, hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. ila kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.

Huu ndio wimbo wake wa kwanza kutoka, na utakuwa katika album yake ya kwanza ambayo bado tunaendelea kuirekodi. Video ya wimbo huu imekwishafanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo.


SONG'S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Contacts: C-SIR MADINI: 0712-719004
KID BWOY: 0713-131073

KUSIKILIZA NYIMBO ZOTE ZA BONGOFLAVA INGIA BONGO STARLINK BLOG

Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive