RATIBA YA SANYA SANYA WEEK END HII
Ijumaa ya tar 27 May LADY JAYDEE na Machozi Band watakuwepo Mzalendo PubBeba Shangwe mfukoni na raha kiunoni, hakuna kukaa chini kwenye viti
Jumamosi Lady JayDee na Machozi Band watakuwepo The Arcade - Mikocheni kujumuika na kufurahia pamoja na wapenzi wa football baada ya Match ya Fainali ya UEFA Champions League kati ya Manchester United na BarcelonaYANAYO ENDELEA NYAMONGO
WASHINDI WA SHINDANO LA KUHESABU SHOWS ZA JAYDEE & MACHOZI BAND ZILIZOPITA
Ndio alikuwa wa kwanza kupatia idadi ya shindano la shows zilizopita na kupata 750,000/= Shilingi za Kitanzania
Mshindi huyu wa pili alipata 250,000/= shilingi za Kitanzania
Ana complimentary ya kuhudhuria shows zote popote hata akipenda kuja na Machozi Band safari atalipiwa kila kitu kwa mwaka mzima.
Sasa basi, baada ya hayo yoooote linakuja shindano lingine
This time zawadi itakuwa kubwa zaidi ya hiyo iliotoka mwanzo.
Nitatoa idadi ya show itakayo anzia Alhamis ya tar 26 May 2011
Na kuanzia hapo mtatakiwa muendeleze hesabu hadi kuja kufikia fainali ya shindano hili.
Tukijaaliwa uzima Alhamis ya tar 26 May 2011 itakuwa ni show ya 66 Tangu mwaka kuanza.
Itakapofika December 31, 2011 Tutapost picha za show yasiku hiyo na mtatakiwa kutujuza itakuwa ni ya ngapi.
Na kuanzia hivi sasa shows zote zitakuwa zina postiwa katika blog ili msikosee mahesabu
Kila heri katika shindano hili jipya.
Zawadi zitatangazwa zitakapokuwa zimekamilika. Tunaziongeza ukubwa na wingi
HABARI NJEMA KWA WASANII CHIPUKIZI WA KIZAZI KIPYA
Je wewe ni msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya?
Umerekodi wimbo wako lakini haupigwi redioni?
Unaamini wimbo wako ni mzuri na unaweza kuwakamata mashabiki?
Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako, Kampuni ya PROMO MEDIA ENTERTAINMENT ni waandaaji wa kipindi kipya cha redio
“CLUB BONGO “. Kipindi kitaanza kurushwa rasmi tarehe 04/06/2011 kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne kamili usiku kupitia PASSION FM. Na kitakuwa kikikujia hewani kila siku ya jumamosi saa tatu hadi saa nne kamili usiku.
Kipindi hiki ni kwa ajili ya kupromoti nyimbo za wasanii chipukizi wenye nyimbo nzuri lakini wameshidwa kuzipeleka redioni..
Leta wimbo wako katika ofisi zetu, Ofisi zetu zipo nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA BUILDING…
Leta wimbo wako mapema, wasanii watakao leta nyimbo zao mapema ndio watakao pata nafasi ya kwanza kupigiwa nyimbo zao redioni…
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba
0652458398 AU 0788363058..
Kwa walioko nje ya Dar es salaam, Tuma kazi yako kwenda kwa:
Managing Director,
PROMO MEDIA ENTERTAINMENT
P.O.Box 35967
Dar es salaam.
PROMO MEDIA ENTERTATINMENT, MKOMBOZI WA WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA.
ZIARA ZA MH.MAKALLA SEHEMU MBALI MBALI
MSAADA WA MABATI 40 NA SARUJI 40 UJENZI WA KITUO CHA POLISI TURIANI.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Turiani, Wilayani Mvomero , ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) saruji mifuko 40 na bati 40 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Turiani, ambapo ujenzi wake umekuwa ukisuasua tangu mwaka 2003 , vifaa hivyo vinathamani y ash: milioni 1.5
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Polisi Turiani, Wilayani Mvomero ,akiongozwa na ( ASP), Rajabu Shemndolwa ( kulia) , ujenzi wa Kituo hicho umesuasua tangu mwaka 2003 , hivyo Mbunge huyo ametoa msaada wa bati 40 na saruji mifuko 40 , vyote vikiwa na thamani y a sh: milioni 1.5
MSANII MPYA C-SIR
Mambo vipi,
Nachkua nafasi hii kukushkuru sana kwa support unayoendelea kutupatia kiukweli bila mchango wako hatuwezi fika popote.
Sisi kama TETEMESHA RECORDZ tumejiwekea malengo ya kuwa tunajaribu kutafuta wasanii wachanga kabisa lakini wenye vipaji na kuwapika kisha kuwatambulisha katika music industry hapa TZ.
Tulianza na HUSSEIN MACHOZI, akafuata SAJNA na sasa ni zamu ya msanii mwingine mpya C-SIR MADINI kutoka Mwanza.
Huyu tunaemtambulisha sasa jina lake kamili ni PETER MPONEJA, na jina lake lingine la nyumbani ni MASISA, hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. ila kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.
Huu ndio wimbo wake wa kwanza kutoka, na utakuwa katika album yake ya kwanza ambayo bado tunaendelea kuirekodi. Video ya wimbo huu imekwishafanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo.
SONG'S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
Contacts: C-SIR MADINI: 0712-719004
KID BWOY: 0713-131073
KUSIKILIZA NYIMBO ZOTE ZA BONGOFLAVA INGIA BONGO STARLINK BLOG

