Diet "DAY 17"

  • Asubuhi shughuli ya kwanza ni kukimbia saa 1
sit ups 60 -65

Maji moto glass 4



Breakfast: 1 Glass ya juice ya Nanasi ukiamua kula hata na nanasi lenyewe pia

Cornflakes na maziwa "Kipimo kiwe cha wastani"

Coffee au Tea kikombe kimoja chenye 1 sugar

2 fried eggs "tumia olive oil au mafuta ya alizeti kijiko kimoja tu"













Kipindi cha mchana kikifika pia unatakiwa unywe maji moto glass 4

Kabla, au baada ya mlo



Lunch: BBQ Fish, Salad na ndizi moja ya kuchoma



Jioni wakati jua likizama unatakiwa kukimbia muda wa saa 1 nzima

na kufanya sit ups 60 -65.

Unatakiwa vile vile kunywa maji moto glass 4



Dinner: 2 toasted white bread na supu ya Vegetables







SHAMBA - Hii waga ipo tu, haiko kwenye album yoyote ya JayDEE

JIDE wa 2005" Album (MOTO) Song- Rafiki wa Mashaka

DIET IMENIFIKISHA HAPA SIKU YA 16, WIKI YA PILI NITAWEKA PICHA ZAIDI ZA KUONYESHA MWILI KWA UKARIBU Mjue kama inafanya kazi au la!!

Eid Mubarak, karibuni Nyumbani Lounge kwa muziki murua pamoja na story za hapa na pale.



Ikiwemo chakula na vinywaji mbali mbali











ITAZAME TU NA HII







URBAN PULSE CREATIVE wakishiriana Miss Jestina Blog

VOTE FOR SHAA





The Team



Kutoka kushoto ni Marc Heijnen, Denis Fulgence na Henry Kapinga


Hicho ndicho kikosi kazi cha Delmore Company - Africa.
Kampuni ya Delmore ni wawakilishi wa Mauzo wa Product za Philips na NEC kutoka Ulaya; Makao Makuu yake yapo Netherland na Branch ofisi kwa Afrika ipo Dar es salaam Tanzania.
Makampuni yote ambayo yana uwezo wa kuwa Partner/Distributor wa Products za Philips au NEC wanaweza wakafanya mawasiliano kwa:-
Namba +255 778 020 747
au tembelea website yetu www.delmorecompany.com





Diet "Day 16" KWENYE SIKUKUU NAJUA MTA SKIP, Ila mkiisha maliza kupakia mahanjumati mnaweza kurudi kuendelea





Asubuhi ni kukimbia kwa mwendo pole muda wa saa nzima


Sit-ups 50 - 60

Glass 4 za maji moto yaliokamuliwa ndimu au limao



Breakfast: 1 glass of milk "LOW Fat"

1 Toasted brown bread

1 Boiled sausage

na Fruits za aina mbali mbali





Lunch: 1/4kilo ya nyama ya kuchemsha

Unaweza kuifanya kama mchemsho tu wa kiswahili, ukatupia na kabich, njegere, karot, hoho na vinginevyo vya kuongezea ladha, bila kuweka mafuta lakini

Kiazi kimoja kikubwa cha kuchemsha



Au ukala mchemsho wa kuku "Chagua kimoja wapo

Na salad au mboga zozote za majani zilizopikwa kwa kuchemshwa bila mafuta

Usiache kunywa maji moto glass 4

Glass 1 ya Mango Juice



Jioni unakimbia tena saa nzima, unafanya sit ups za kutosha

Maji moto glass 4



Dinner: BBQ Chicken 1/4 Kuku, ndizi 1 ya kuchoma na Salad







FUTARI ZA MWISHO MWISHO KABLA YA SIKUKUU YA EID

Famille nombreuse, kutoka kushoto Cute Smile, Maggie, Mdau, Sophia, Faraji na Imma "TheDesigner"



Hapa kaongezeka Captain na Sab mwenye baibui jeusi











Rafiki, Ester Ulaya na Sabina wote wenye t-shirts nyeupe



Shughuli hii ilifanyika Shopaz Plaza na host alikuwa Bw.Faraji Mohamed





SIKU YA EID MACHOZI BAND ITAPIGA NYUMBANI LOUNGE



Eid Mubarak na karibuni sana



Shukrani kwa Hamisi Samuli kwa kadi ya Eid





TANGAZO....KUTOKA MARIAN SCHOOLS BAGAMOYO



Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising hii

ya Kujenga na kuendeleza Shule hizi.


Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba



Wazazi,wanafunzi wa zamani,wenyeji wa Bagamoyo na wote wale wenye Mapenzi mema mnakaribishwa sana sana tarehe 4th SEPT Diamond Jubilee Hall saa Moja jioni.


Asanteni!



Diet "Day 15" Nimeonelea swala la Baiskeli litakuwa gumu kidogo kwahiyo tuliache kwanza



Asubuhi ya siku ya 15 unatakiwa utembee au kukimbia kwa polepole kwa wastani wa saa nzima

Ukirudi unafanya sit-ups 50 -60

Unakunywa maji moto glass 4

Unakunywa kikimbe kimoja cha chai au kahawa chenye 1 kijko cha sukari



Toasted brown Brean 1 Slice

1 Boiled egg

1 Glass of Orange Juice





Katika maongezi ya kusubiria lunch badala ya kunywa bia unatakiwa unywe maji moto glass4

Lunch: inakuwa ni mishkaki 3 ya beef au kuku

Wali kipimo cha kikombe kimoja na sio zaidi

Na Mboga mboga za majani



Jioni pia utatakiwa utembee au ukimbie kwa polepole muda wa saa nzima

Baada ya hapo unafuatia na sit-ups 50 -60

Maji moto glass 4



Dinner ni nusu samaki wa kuchemsha

Njegere na glass moja ya Carrot juice









I LOVE THE JACKET AND THE POSE





MACHOZI BAND SHOW!!!!!!

Ijumaa ya tar 26 August 2011

Show ilikuwepo kama kawaida Nyumbani Lounge



Jumapili ya tar 28 August 2011

Pia Machozi Band ilipiga Nyumbani Lounge



Tutawaletea taarifa ya ratiba za sikukuu kama patakuwa na mabadiliko yoyote ya Venue



Heri ya Sikukuu in Advance



GROOVEBACK......."Nyumbani Lounge" Every Saturday





Amos Makalla aingilia MGOGORO WA ARDHI KIPERA



Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akimsikiliza Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kwa Mbunge wake juu ya kitendo cha kubomolewa choo chake na Mwekezaji Raia wa kigeni na kuzungusha uzio uliofikia upenuni mwa makazi yake. Mbunge huyo alitembelea kitongoji hicho mwishoni mwa wiki kujionea hali halisi ya mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Mkoani Morogoro, Amos Makala (kushoto) akikagua uzio uliowekwa na Kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa na Mzungu aliyenunua shamba Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero na kuzua mgogoro mkubwa wa mipaka baina yake na wananchi wa eneo hilo. Anaemuongoza ni Said Ahmad mkazi wa Kinyenze



Na: Mroki Mroki, Mvomero

MBUNGE wa jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, Amos Makala ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo katika Kitongoji cha Kinyenze , Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali , Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baina ya wananchi na mwekezaji wa Kigeni aliyeuziwa shamba kijijini hapo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Kijijini hapo Makala aliyeambatana na Ofisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Majaliwa Jaffari amewataka idara ya ardhi kuchukua hatua za haraka na dharula kutatua mgogoro huo kabla ya kuibuka kwa machafuko ya uvunjifu wa amani.

“Nimejionea mwenyewe baada ya kusikia kiliochenu juu ya mwekezaji huyu, watu wa ardhi tafadhalini sana lishughulikieni suala hili haraka sana na mkae pamoja mgogoro huu umalizike upesi iwezekanavyo, ndani ya wiki moja tatizo hili liwe limemalizika”, alisema Makala.

Aidha Makala amesema tatizo hilo likiendelea ataungana na wananchi wake kufungua kesi Mahakamani ya kumpinga mwelezaji huyo na amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kutumia mamlaka waliyonayo kufika kijijini hapo wafungue uzio huo uliowekwa na mweklezaji huyo haraka ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali, watoto kwenda shule na watu kuvuna mazao yao yanayoibiwa na walinzi wa kampuni ya Tanbreed Poultry Limited ambayo imemega mashamba yao.

“Katika hili ninaungana nanyi na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wafike hapa wakiwa na dola na kukata uzio huu, ili wananchi muendelee na shughuli zenu za kijamii, si haki kufunga barabara mnayoitumia kwenda katika makazi yenu na mashambani, hili lisipofanyika tutatafuta mwanansheria na kufungua kesi ya Mahakamani ya kumpinga mwekezaji huyu”,alisema Mbunge Makala.

Makala pia aliwapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kuwa watulivu pasipo kufanya vurugu katika kipindi kirefu tangu kuibuka kwa mgogoro huo bila kupatiwa ufumbuzi kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu licha ya kuandikiwa barua tangu mwezi Aprili mwaka huu mgogoro huo ulipoanza kushika kasi.

“Wananchi mmefanya jambo jema sana la kuheshimu mamlaka za kisheria kwa kuwa watulivu kipindi chote lakini vinginevyo hapa machafuko yangetokea maana wananchi mpo wengi kuliko hao askari wao wanaolinda hilo shamba”, alisema Makala.

Pia alisema kwa maelezo aliyoyasikia kutoka kwa baadhi ya wazee wa kijiji hicho Ally Kidunda na Said Ahmad na viongozi wa Kijiji yaliyotolewa kwaa nyakati tofauti Mwekezaji huyo ndiye mvamizi wa eneo lao na si wananchi maana hata kijiji hakimtambui kwa maana hajawahi kufika kwao.

Nae Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jaffari alisema watalishughulikia suala hilo haraka na hasa baada ya kufika eneo la tukio na kukiri kuna mapungufu katika ramani waliyonayo.

Agosti 23, mwaka huu wananchi hao waliitaka serikali kuingilia kati mgogoro huo haraka kabla ya machafuko kutokea wakati wakiwa katika mkutano wa hadhara uliokuwa uhudhuriwe na Mkurugenzi wa Wilaya na Maofisa wa Ardhi.

Mwisho.



Diet "DAY 14"

Kuanzia asubuhi ni mazoezi kukimbia na sit-ups

Kikombe kimoja cha chai, au kahawa

Maji moto glass 4



Mchana ni SALLADDY tu a.k.a Kachumbari

Maji moto glass 4



Jioni kukimbia na Sit-ups

Maji moto glass 4

Matunda ya kutosha





Diet "DAY 13"

Itakuwa ni week end si ndio Unaweza ukafanya sit -ups nyingi tu ukiamka kama utashindwa kuwahi kutembea Kikombe kimoja cha Chai au kahawa chenya kijiko kimoja cha sukari Ndizi mbivu 1 Maji moto glass 4







Lunch ni Chapati moja na Supu ya Kuku wa Kienyeji hakikisha umetoa ngozi kwenye kuku

Maji moto glass 4 pia na embe 1



Jioni unaweza ku skip kutembea na sit ups pia kwakuwa kusema kweli week end ni ngumu wenzio wamekaa mahala wewe unyanyuke uende kuanza mazoezi

Hapa unaweza ukategea lakini usizoee sana



Maji moto kabla hujaanza chochote jioni Glass 4

Katika mazingira yoyote utakayokuwa kula mishkaki 3 tu ya samaki na Salady

Glass za wine zisizozidi 2 kwa usiku mmmoja









Good night



TANGAZO......



pole na kazi dada


naomba unisaidi kunitangazia katika blog yako nimepotelewa na bahasha iliyokuwa na vyeti ndani ya daladala ya mwenge kwenda k'koo kupitia barabara ya sinza ndani kulikuwa na vyeti hivi leaving certificate ya form four na form six,cheti cha ukwata o'level na A' level, result slip,certificate of secondary education ya O'level,cheti cha kuzaliwa,na cheti cha computer,



vyeti yote hivyo vinasomeka kwa jina la VENANCE LUSINDE...na kulikuwa na DVD ya sendoff iliyo andikwa Mariamu.vimepotea tar 24/8


kwa yoyote atakayepata naomba tuwasiliane nami kwa namba hizi
0787 514920
0655 514920
0659 437711




ahsante kwa ushirikiano wako .



USAFIRI MPYA WA MACHOZI BAND......."MUNGU NI MWEMA"



Picha zaidi likishabandikwa Chata

Asanteni kwa kuendelea ku support



PIGIA KURA WATOTO WA TANZANIA WARUDI NA USHINDI NYUMBANI

Shaa



AY



CPWAA



Let's support our Bongo artists by VOTING... 2011 Channel O Music Video Awards. Go to the following links and cast your votes:



1. Shaa: http://channelo.dstv.com/artist/shaa/



2. AY: http://channelo.dstv.com/artist/ay-ft-ms-triniti/

...

3. C-Pwaa: http://channelo.dstv.com/artist/cpwaa-ft-various-artists/





TANGAZO..........



A bi monthly magazine from Tanzania Private sector Foundation TPSF!

For information sharing with all stakeholders including

business community, producers, traders and exporters development partners, government and government support institutions, processors groups and general public,

For easy access to business information, get your copy!

Tanzania Business Focus delivers the information and insight you need to take control of your business, your finances, and your future.

Tanzania Business Focus coverage goes beyond the headlines and behind the scenes. It delivers what you want and what you need to know.

TPSF is proud to present, Tanzania Business Focus! Power of the Private Sector!

GET YPUR COPY FROM ALL THE LEADING SUPER MARKETS IN DAR ES SALAAM, ARUSHA, MOSHI, DODOMA, AND SOON IN MWANZA AND MBEYA. YOU ARE ASLO WELCOME TO CONTRIBUTE ARTICLES AND OR ADVERTISE FOR ALL OUR FUTURE ISSUES.

For inquiries and advertisements please contact info@tpsftz.org and info@eurocom.co.tz





TANZANIA MUSIC TELEVISION



TANGAZO

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WANAOISHI NDANI NA NJE YA TANZANIA

KATIKA SIKU ZIJAZO ZA KARIBU TUTAFUNGUA TELEVISHENI. CHANELI YA MUZIKI WA

KITANZANIA, KWA JINA LA TANZANIA MUSIC TELEVISION {TMTV} (WWW.TMTV.CO.TZ) AMBAYO

ITAKUWA INAPATIKA KWENYE MTANDAO,SETILATI,SIMU ZA MKONONI NA

VING'AMUZI(DECODER)

CHANELI HII ITAKUWA NA VIPINDI VIFUATAVYO:

1.BONGO BOX

2.SALAMU BOX

3.BENDI ZETU

4.TAARABU

5.ZILIPENDWA

6.NYIMBO ZA DINI

7.VIPAJI

8. HABARI ZA MUZIKI

9.SWAHILI HIP-POP

10.NYIMBO ZA UTAMADUNI



ILI KUBORESHA UFANISHI WA CHANELI TUNAOMBA MAPENDEKEZO YENU KUPITIA:

info@tmtv.co.tz
BONYEZA HAPA KWA KUANGALIA CHANELI
KWA KOMPYUTA NYINGINE UTALAZIMIKA KUDOWNLOD SOFTWARE YA MICROSOFT SILVER LIGHT KWA AJILI YA KUANGALIA TV.
SOFTWARE ITAJITOKEZA KTK SCREEN KWA AJILI YA KUDOWNLOD.



WENU



UTAWALA

TANZANIA MUSIC TELEVISION



COASTAL UNION YAPATA MSAADA





.



KLABU ya Coastal Union ya Jijini hapa imepokea msaada wa vifaa vya

michezo vyenye thamani y ash 2 milioni kutoka kwa mdau wa michezo

nchini Mohamed Bawazir ikiwa ni mchango wake wa kuiwezesha kushiriki

vyema ligi kuu vodacom.



Vifaa hivyo ni jezi,mipira,beeps soks jezi za walinda mlango kwa ajili

ya wachezaji pamoja na vifaa vya uhamasishaji vya kutumiwa na

mashabiki ambavyo ni vuvuzela na tambara la hamasa.



Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika jana asubuhi katika hoteli ya

Tanga Beach Resort ambapo clabu ya Coastal iliwakilishwa wapenzi wake

wakiongozwa na Mwenyekiti wao,Ahmed Aurora na Makamu mwenyekiti

Steven Mguto.



Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Bawazir alisema lengo ni

kutoa hamasa kwa wadau wengine kujitolea kuisaidia Coastal Union

inayokabiliwa na michuano ya Ligi kuu Vodacom pamoja na kuendeleza

michezo kwa ujumla katika mkoa wa Tanga.



“Nimeamua kuongoza njia ili wadau wengine wajitokeze kusaidia kuhuisha

michezo katika mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa ikiwika katika miaka ya

nyuma kwenye michezo mbalimbali”alisema Bawazir.



Mdau huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd ya

jijini Dar es salaam,alisema kuna kila haja kwa wadau wa Tanga walioko

maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia.



Vifaa vilivyokabidhiwa ni sare jozi moja,seti mbili za sare za walinda

mlango ,soks pea 20,jezi za mazoezi jozi 30,mipira mitatu aina ya

jabulani,bendera na tambara kubwa la hamasa.



Mwenyekiti wa klabu hiyo,Aurora alimshukuru mdau huyo kwa mchango wake

mkubwa ambapo alisema vifaa hivyo vitawasaidia wachezaji pamoja

mashabiki wakati wa michuano yote inayoikabili timu hiyo.



“Bawazir amekuwa mdau wa kwanza kuisaidia klabu yetu ukiacha wadhamini

wakuu,tangu tumechaguliwa tumekuta Coastal haina vifaa wala chochote





Popular Posts

Popular Posts

Followers

Search This Blog

Blog Archive